Atabatu Abbasiyya tukufu yazindua nyumba za Abbasi (a.s) za makazi, na kitengo cha miradi ya kihandisi chasema zimejengwa kwa usanifu wa kisasa..

Maoni katika picha
Alasiri ya Juma Nne (8 Dhulqa’adah 1438h) sawa na (01 Agosti 2017m) katika jengo la Shekh Kuleiniy, ilifanyika hafla ya uzinduzi wa nyumba za Abbasi (a.s) zilizo jengwa kwa ajili ya makazi ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, hafla hiyo ilihudhuriwa na watu wengi wakiwepo wageni mbalimbali pamoja na waandishi wa habari wa luninga (tv) redio na magazeti bila kuwasahau wanufaika wa mradi.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu halafu ukafuatia wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya na ikasomwa surat Fat-ha watu wakiwa wamesimama kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu wa Iraq, kisha ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika ndugu zetu watukufu wanao zitumikia Ataba takatifu, na kuchagua kumtumikia Sayyid Shuhadaa (a.s) na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wamechagua jambo jema sana hapa duniani kwa kujitolea kufanya kazi katika Ataba hizo takatifu na kuwahudumia mazuwaru watukufu, ikawa ni wajibu kwa uongozi wa Atabatu Abbasiyya ufanye kila uwezalo kwa ajili ya watumishi hawa, ndipo ukaamua kujenga mradi huu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu baada ya miaka mitatu ya kupambana na kuhangaika, hatimae mradi umekamilika; sasa watumishi wetu watukufu watapata nyumba bora za makazi yao na familia zao”.

Kisha ukafuata ujumbe wa wasimamizi wakuu wa mradi ambao ni kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na rais wa kitengo cha uhandisi; Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, alielezea hatua muhimu ambazo mradi wa nyumba za Abbasi (a.s) ulipitia pamoja na mambo ya kitaalamu yaliyopo katika mradi huu.

Halafu ukafuata ujumbe wa shirika lililo tekeleza mradi, ambalo ni shirika la ujenzi la Sibtwain ulio wasilishwa na mkuu wa shirika hilo Ustadh Maahir Abdul-ameer, alifafanua kua: “Hakika mradi huu ni moja ya mambo makubwa katika mji mtukufu wa Karbala kwa sababu ni mradi wa kwanza mkubwa wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa kiwango cha juu uliotekelezwa na wairaq wenyewe, kuanzia wazo, usanifu na ujenzi bila kushirikisha mashirika ya nje ya nchi”.

Hafla ikapambwa na qaswida ya kimashairi iliyo somwa na mshairi Sayyid Adnan Mussawiy mjumbe wa kamati ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya, beti zake zilimsifu Abulfadhil Abbasi (a.s) na utumishi wake, na Muhammad Tamimi akasoma shairi lenye beti za maelekezo ya kidini.

Baada ya hapo wahudhuriaji wote wakaelekea katika shughuli ya kukata utepe kama ishara ya kuzinduliwa rasmi kwa nyumba hizo, huu ni mradi wa kwanza wa nyumba za makazi zilizo jengwa katika mkoa wa Karbala kwa kiwango hiki.

Kulikua na kipengele cha upigaji wa kura kwa ajili ya kugawa nyumba za makazi kwa watumishi kilicho gubikwa na furaha kubwa na wakatoa shukrani za dhati kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupata zawadi hii na wakaahidi kuendelea kumtumikia kwa ikhlasi na kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wake watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: