Utekelezaji wa mradi wa kituo cha kiislamu cha masomo ya mikakati unaenda kama ulivyo pangwa..

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha uhandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesisitiza kua: “Kazi ya ujenzi wa jengo la mradi wa kituo cha kiislamu cha masomo ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya inaendelea vizuri kwa kufuata muda ulio pangwa, mradi huu unatekelezwa katika mji mtukufu wa Najafu, kuendelea vizuri kwa utekelezaji wa mradi huu kunatokana na ustadi pamoja na ikhlasi ya watendaji, kuanzia shirika lililo pewa tenda ya ujenzi na wasimamizi wa mradi kutoka katika kitengo chetu, tunatarajia kua jengo la mradi huu litakua zuri na litavutia”.

Akaongeza kua: “Tayali tumepandisha jengo lote kama lilivyo chorwa, tumefika zaidi ya asilimia 90% katika unyanyuaji wa jengo, kazi hii imefanyika mfululizo pia imeenda sambamba na kumwaga zege katika kila ghorofa”.

Akaendelea kusema kua: “Hali kadhalika ujenzi huu unafanywa pamoja na ujenzi wa miundo mbinu ya usambazaji wa maji, ambapo pia miungo mbinu mingine itafuata, baada ya kukamilika ujenzi huo, itafuata hatua ya ufunikaji wa ukuta (plasta) na kuweka madirisha na milango pamoja na mambo mengine yanayo hitaji kutengenezwa kwa umaridadi”.

Kumbuka kua mradi huu unatekelezwa na shirika la ujenzi la Anwaarul-Hadhar, ukubwa wa eneo linalo jengwa ni mita (890) na jengo linalo jengwa ni ghorofa saba, jengo hili litatiwa nakshi zinazo endana na hadhi ya kituo hiki pia zitakazo himili mazingira ya sasa na ya baadae.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: