Atabatu Abbasiyya tukufu yaanza ujenzi wa kituo cha elimu katika mkoa mtukufu wa Najafu na yasisitiza kua kitakua cha mfano na kuchuana na vituo vya aina hiyo vya kitaifa na kimataifa…

Maoni katika picha
Miongoni mwa miradi yake ya kielimu hapa Iraq, na kufuatia maendeleo ya elimu yanayo shuhudiwa na ulimwengu wa sasa, Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kujenga kituo cha elimu katika mji mtukufu wa Najafu, kitakacho kua na vyuo kadhaa vya masomo ya muda mfupi na muda mrefu, kituo hicho ni zao la Atabatu Abbasiyya linalo tokana na chuo cha Alkafeel kilichopo katika mji wa Najafu, kilicho pata mafanikio makubwa na sifa nzuri kwa muda mfupi, kutokana na uzuri wa ratiba za masomo zinazo endana na taasisi za kisekula za kimataifa, na kutumia njia bora za ufundishaji sambamba na kua na vifaa vya kisasa vya kusomea, pamoja na udogo wa jengo lake lakini wamefanya kazi kubwa na matunda yameonekana, kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechukua jukumu la kupiga hatua ya pili kwa kubadilisha chuo (kitivo) kua chuo kikuu, Jamabo hilo linahitaji upanuzi wa majengo yake.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao ndio wasanifu na wasimamizi wa mradi huu, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh alipo kutana na mtandao wa Alkafeel katika eneo husika alisema kua:

“Mradi huu unatekelezwa katika uwanja unaokadiriwa kufika mita za mraba (8000), na umesanifiwa na kituo cha masomo na utafiti Alkafeel kilicho chini ya kitengo chetu, maamuzi ya kutekeleza mradi huu yalipatikana baada ya kukaa mara kadhaa na wanufaika wakuu wa mradi ambao ni kitengo cha malezi na elimu ya juu na chuo cha Alkafeel, baaba ya vikao hivyo tulibaini majengo wanayo hitajika kwa ajili ya vyuo vyao na majengo ya idara, baada ya kupatikana muwafaka mradi ulianza kwa kuandaa michoro na kusanifu majengo, kazi hiyo ilifanywa na shirika la Liwaau Al-Aalamiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi inatekelezwa ndani ya muda uliopangwa na uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, inahusisha kujenga vyuo viwili ambavyo vinatarajiwa kufunguliwa katika mwaka ujao wa masomo, pia watajenga maktaba, nyumba za chini, mabustani na sehemu zingine za majengo zitakamilika kwa muda ulio pangwa.

Akaongeza kusema kua: “Kazi inayo endelea sasa hivi ni ujenzi wa vyuo viwili katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (1700), panajengwa ghorofa nne, ambazo zitakua na vyumba vya madarasa, maabara na ofisi, ujenzi unaendelea kama ulivyo sanifiwa (pangwa), ujenzi unafanyika kwa kutumia vifaa vya kisasa kuanzia katika msingi hadi kukamilika kwa jengo, hadi sasa jengo limefika ghorofa la tatu, na jengo lingine lipo katika hatua ya msingi, sambamba na ujenzi huu pia kuna ujenzi wa fensi (ukuta) wa nje wa kuzunguka majengo yote pamoja na kutengeneza barabara zake”.

Rais wa kituo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu dokta Abbasi Didah amesema kua kituo hiki cha elimu kitakua bora kabisa na kitatoa ushindani mkubwa kwa vituo vingine vya aina hii vya kitaifa na kimataifa, kitafuata utaratibu mzuri na kuchuana na vyuo vingine katika kutoa elimu bora na kutumia akili na vipaji vya wanafunzi wetu.

Akaongeza kusema kua: “Kituo hiki kinajengwa kwa mujibu wa mpango kazi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kuanzishwa kwa taasisi za malezi na elimu, hivisasa ni wakati wa kujenga majengo yanayo endana na taasisi hizo, jengo hili ni moja ya utekelezaji wa mpango huo”.

Akabainisha kua: “Kutokana na juhudi za uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, chuo cha Alkafeel kitabadilishwa na kua chuo kikuu kikubwa hapa Iraq, hilo litafanyika kwa kubadilisha muundo wa idara zake na kuzifanya kua michepuo (vitivo) vya chuo, na sasa hivi unashuhudiwa ujenzi wa majengo ya vitivo hivyo vitakavyo kua chini ya chuo kikuu hiki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: