Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesisitiza kua: “Kubba la Maqamu Swahibu Zamaan (a.f) katika Masjid Sahla litajengwa kisasa katika ubora mkubwa, unao endena na utukufu wa mwenje jina hilo kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine ubora unao endana na ujenzi wa kisasa, ikumbukwe pia huo ni msikiti mkongwe zaidi katika misikiti ya Iraq, watalamu wetu wanafanya kila wawezalo kwa ajili ya kukamilisha mradi huu ndani ya muda ulio pangwa”.
Akaongeza kusema: “Tulianza hatua ya kwanza iliyo tanguliwa na upauaji katika eneo tukufu la kubba, nayo ni hatua ya kuweka vifuniko vya dhahabu, ambapo jumla ya kilo tatu (kg.3) zimetumika, vifuniko hivyo vilitengenezwa na idara ya dhahabu na alminiam chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi, baada ya kuchukua vipimo kwa umakini mkubwa na kisha kuanza kuvitengeneza kwa kutumia njia ya ngozi ambayo vifuniko vyake hua na uimara mkubwa sana, njia hiyo imeonyesha mafanikio makubwa katika kazi zoto zilizo fanywa ndani au nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kukamilisha hatua hii wataendelea na hatua inayo fuata ambayo ni kuweka Kashi Karbalai”.
Akabainisha kua: “Katika uwekaji wa vifuniko vya dhahabu tumetumia njia ya kitalamu zaidi ambayo imesha onyesha ufanisi mkubwa tofauti na njia iliyo kua ikitumiwa zamani, njia ambayo huvifanya vifuniko hivyo vidumu kwa muda mrefu sana na huvifanya vishikamane sana na ukuta wa kubba tukufu”.
Akaongeza kua: “Sisi tunajivunia mafanikio haya yanayo tokana na kazi ya wairaq halisi, na anaye faa kupongezwa zaidi ni Atabatu Abbasiyya tukufu, kazi hii ni muendelezo wa kazi zingine kama hizi walizo fanya kuanzia minara ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi minara ya malalo ya Sayyid Muhammad (s.a) pamoja na kubba ya Maqamu Imamu Mahdi (a.f) katika mji mtukufu wa Karbala”.
Katibu mkuu maalumu wa Masjid Sahla dokta Mudhar Madani amebainisha kua: “Jambo kubwa tunalo zingatia katika ujenzi wa kubba hili ni ubora, kwani linamuwakilisha Imamu aliye hai, hivyo tumejitahidi kulisanifu kisasa zaidi na kulifanya kua tofauti na kubba zingine zilizo zoeleka katika Ataba mbalimbali, kuanzia uwekaji wake wa dhahabu na hata kashi karbalai”.
Kumbuka kua utekelezaji wa mradi huu upo ndani ya mfumo wa ushirikiano wa kiufundi kati ya Atabatu Abbasiyya na Ataba zingine pamoja na mazaru takatifu, ujenzi huu umeanza baada ya kupata mafanikio makubwa katika miradi ya aina hii iliyo tekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na baada ya kupata uzowefu mkubwa katika sekta hii, unao lingana au kuzidi mashirika ya kigeni ambayo hufanya kazi hizi.