Atabatu Abbasiyya tukufu yazindua mradi wa kituo cha kibiashara cha Afaaf, na yasema ni mradi wa pekee na yatoa wito wa kunufaika na huduma zake…

Maoni katika picha
Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya ujenzi ulio fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha miradi ya kihandisi kilicho fanya kila kiwezalo ili kukamilisha mradi huu ndani ya muda ulio pangwa na kwa ubora wa hali ya juu unao endana na maendeleo ya sekta hii, asubuhi ya Juma Mosi (13 Rajabu 1439h) sawa na (31 Machi 2018m), umefanyika uzinduzi wa kituo cha kibiashara cha Afaaf, ambacho ni moja ya miradi ya kiuchumi ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na ambacho kinatarajiwa kutoa huduma za kibiashara kwa wakazi wa Karbala na mazuwaru watukufu, huu ni mradi mpya wenye mvuto kibiashara unao fungua milango yake kwa mara ya kwanza, utakao kua mbali na ghushi pamoja na alama feki za kibiashara, jambo hili limezingatiwa kuanzia katika usanifu wa kituo hiki.

Uzinduzi wa kituo hiki umefanyika sambamba na maonyesho makubwa ya Atabatu Abbasiyya tukufu yaliyo hudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, pamoja na marais wa vitengo vya Ataba na ugeni rasmi ulio wakilisha Atabatu Husseiniyya tukufu, bila kuwasahau wawakilishi wa serikali kutoka katika mkoa wa Karbala, wakiongozwa na Muhandisi Jaasim Khatwabi rais wa baraza la mkoa na idadi kubwa ya wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu –ambao ndio wasanifu na wasimamizi wakuu wa utekelezaji wa mradi huu- Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Daima uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umekua ukitoa msaada mkubwa kwa mradi wowote unaolenga kuhudumia watu, na kufanya kila kinacho weza kuboresha mazingira ya taifa kwa ujumla bila kusahau mazingira ya Karbala, mradi huu unaingia katika malengo ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuwahudumia watu wa Karbala na mazuwaru wanaokuja kutembelea Ataba mbili tukufu na watakao penda kununua bidhaa katika kituo hiki, ambacho kipo umbali wa (km 1.5) kutoka katikati ya mji wa Karbala, katika eneo la wazi (kitongoji cha Hussein “a.s”).

Akaongeza kusema kua: “Mradi huu umetekelezwa kwa kufuata vigezo vya kimataifa, ndio vilivyo zingatiwa na shirika lililo tekeleza mradi huu, ambalo ni shirika la ujenzi la ardhi tukufu, nalo ni shirika la kiiraq lilibeba jukumu la kutumia teknolojia ya kisasa zaidi inayo tumika kwenye ujenzi katika nchi za ulaya, hiki ni kituo cha kwanza kujengwa kwa sifa hizi hapa Karbala”.

Akabainisha kua: “Mradi huu umejengwa katika uwanja wenye ukubwa wa (2m2600), na jengo lina ghorofa tatu, na lina sehemu mbili: sehemu ya kwanza ni maalumu kwa ajili ya maduka, na sehemu ya pili ni kwa ajili ya ofisi na stoo, jengo hili lina sistim za kisasa za (Umeme, viyoyozi, zima moto, kamera, tahadhari, intanet, mwanga…) hali kadhalika lina ngazi maalumu za kupandishia bidhaa na za kutumiwa na watu zipo za lifti na za kuslaidi (kuteleza) pamoja na vitu vingine vingi ambavyo vimekifanya kua kituo cha kwanza cha aina hii katika mkoa wa Karbala, tuna toa wito kwa wafanya biashara waje mapema kuchukua maeneo ya biashara, tumeandaa ghorofa la pili kwa ajili hiyo tu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: