Sehemu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa godauni za Atabatu Abbasiyya tukufu yafikia hatua nzuri…

Maoni katika picha
Mradi wa ujenzi wa godauni za Atabatu Abbasiyya tukufu unao itwa (godauni za Alwafaa) umefika katika hatua nzuri, kazi zinaendelea kama zilivyo pangwa.

Mradi unasehemu mbili: sehemu ya kwanza inahusisha ujenzi wa majengo mawili ya ghorofa, jengo la kwanza lina ukubwa wa (2m3000) -upana wa (mt 30) na urefu wa (mt 100)-, na sehemu ya pili inahusisha jengo lenye ukubwa wa (2m2500), mradi huu unasistim ya zima moto na utoaji wa tahadhari pamoja na mitambo maalumu ya kamera za ulinzi, pia kuna njia za ndani, njia za maji sehemu ya vyoo na sehemu za ofisi na vinginevyo.

Mradi huu unatekelezwa na shirika la ujenzi la Liwaaul-Aalamiyyah chini ya usimamizi wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, hakika shirika hilo limefanya kila aina ya juhudi kuhakikisha wanatekeleza mradi kama ulivyo pangwa, tayali umesha fanyika uhakiki wa kazi zilizo kamilika na kuzikuta zinaendana na viwango vilivyo pangwa.

Fahamu kua mradi huu ni sehemu ya miradi inayo tekelezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya godauni na viwanda, inayo lenga maendeleo katika nyanja mbalimbali, mradi huu wa (Alwafaa) unajengwa katika eneo la Ibrahimiyya lililopo kusini ya mji wa Karbala, na unatarajiwa kuambatana na miradi mingine ya ujenzi wa viwanda na godauni kwa maendeleo ya sasa na ya baadae.

Kumbuka kua kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kuanzishwa kwake baada ya kuanguka utawala ulio pita, kimesha simamia na kutekeleza makumi ya miradi mikubwa na mamia ya miradi midogo na ya kati ukiwemo mradi huu, ndani na nje ya Ataba, sehemu kubwa ya miradi hiyo imefanywa na wataalamu wa kiiraq kwa kushirikiana baina ya kitengo tajwa hapo juu na mashirika mengine ya kitaifa nje ya Ataba tukufu, na mara chache sana wameshirikiana na mashirika ya kigeni ya kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: