Kazi ya upanuzi wa Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f) inaendelea vizuri, tena maendeleo yake yanaonekana wazi, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, ambaye amesema kua: “Mafundi na wahandisi wanao fanya kazi katika mradi huu wamepiga hatua kubwa, hakika wamefanya kazi kwa bidii hadi kufikia hatua hii iliyopo leo, ukiwemo ufuatiliaji na usimamizi wa karibu unaofanywa na kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kilicho ondoa vikwazo vyote vya kiofisi na kiutendaji, kampuni inayo tekeleza mradi huu ni kampuni ya ardhi tukufu ya ujenzi ikishirikiana na wanufaika wa mradi huu, kwani nao hawakubaki nyuma katika kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ustadi mzuri unao endana na hadhi ya mwenye jina la sehemu hii”.
Akabainisha kua: “Baada ya kumaliza kuweka zege katika maeneo yaliyo ongezwa kwenye Maqaamu yanayo jumuisha ukumbi maalum wa wanawake wenye ukubwa wa mita (490) takriban, na ukumbi mwingine maalumu kwa ajili ya wanaume wenye ukubwa wa mita za mraba (310), na ukumbi mwingine wenye ukubwa wa mita za mraba (150), tayali ujenzi wa ndani na nje umekamilika na uwekaji wa vifaa maalumu kwa ajili ya kuweka mapambo ya nje, kazi hizi zinafanyika sambamba na kazi zingine za kupaka rangi na kuweka nyaya za umeme pamoja na kuweka sistim ya spika na vitu vingine vinavyo fungamana na mradi huu”.
Akaongeza kusema kua: “Hali kadhalika ujenzi wa umbo la mnara wa chuma utakao wekwa saa tukufu, ambao ni sehemu za ziada katika mradi huu, mnara huo utakua moja ya alima kubwa na unafanana na mnara wa saa uliopo katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Kumbuka kua Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya wa sasa, unapo ingia katika mji wa Karbala kupitia njia inayo elekea katika Maqaamu ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) nayo ni mazaru mashuhuri, Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya matengenezo kuanzia katika kubba hadi mwenye kumbi za haram na maeneo mengine yanayo fungamana na haram, kwa kua sehemu ilipo Maqaamu hauwezi kufanya upanuzi katika pande tatu, imebidi upanuzi ufanyike upande wa mto Husseiniyya, ambao ni upande wa magharibi, kwa kutumia nguzo za zege ambazo juu yake kumejengwa kama daraja, bila kuzuia maji au kubadilisha muelekeo wake hata kidogo, eneo lililo panuliwa linaukubwa wa mita za mraba (1200) na linaunganika na Maqaamu kupitia milango maalumu.