Kiwanda cha Saqaa chapiga hatua kubwa katika kutengeneza dirisha la malalo ya Shekh Mufidi na Shekh Tusi (q.s)…

Maoni katika picha
Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya kupata hazina kubwa ya ufundi wa kutengeneza madirisha ya makaburi matukufu, mafundi wa kiwanda cha Saqaa cha kutengeneza madirisha na milango ya malalo matukufu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya, wanaendelea na kazi ya kutengeneza madirisha mawili, la kaburi ya Shekh Mufidi na Shekh Tusi (q.s) na yamesha fika hatua nzuri, kazi inaendelea vizuri siku baada ya siku, uzuri wa madirisha hayo umeanza kuonekana wazi, chini ya ratiba maalumu iliyo pangwa na kamati inayo simamia kazi hii kwa makubaliano na Atabatu Kadhimiyya tukufu ambao ndio wanufaika wa mradi, na kwa mujibu wa makubaliano ya pande mbili kuhusu kutengenezwa kwa madirisha hayo.

Mtandao wa Alkafeel ulifika kiwandani hapo na kupata maelezo ya kazi zinazo endelea sasa na ambazo zimesha kamilika, tulifanya mahijiano na mjumbe wa kamati ya usimamizi wa mradi huu, makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Bwana Ali Swaffaar ambaye alituambia kua: “Hakika kazi hii tulifikia makubaliano na Atabatu Kadhimiyya tukufu mwishoni mwa mwezi wa Ramadhani (1438h), kutokana na uzowefu walionao mafundi wa kiwanda cha Saqaa katika utengenezaji wa madirisha, hasa baada ya mafanikio makubwa waliyo pata katika kutengeneza dirisha la kaburi ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya makubaliano ya kazi hii, mafundi walianza kufanya usanifu na kuchagua maneno na maandishi, pamoja na kushirikisha wabobezi wa hati ili kuchagua hati itakayo beba dhana ya utukufu walio nao wanachuoni hao”.

Akaongeza kua: “Tumefanya juhudi kubwa kuhakikisha mradi huu unakamilika na kuingia katika orodha ya miradi tuliyo fanya, tumesha piga hatua kubwa, kazi iliyo baki ni kuweka mina na kutia dhahabu”.

Mkuu wa miwanda cha Saqaa Sayyid Naadhim Jaasim Alghurabi aliongeza kusema kua: “Hakika mradi wa kutengeneza madirisha mawili la kaburi ya Shekh Mufidi na Shekh Tusi umefanyika baada ya Atabatu Kadhimiyya tukufu kuona mafanikio ya kiwanda hiki katika utengenezaji wa madiriha, hasa baada ya kutengeneza dirisha la kaburi ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha tukatengeneza mlango wa malalo ya Sayyid Muhammad Sab’u Dujail (a.s), na kazi zingine nyingi tulizo fanya, kazi hizo ziliifanya Atabatu Kadhimiyya ituamini na iwe na uhakika wa kukamilisha mradi huu kwa mafanikio”.

Akaongeza kua: “Madirisha mawili hayo pamoja na udogo wake lakini yana vitu vingi vya kiufundi, kila dirisha lina urefu wa mita mbili na sentimita sitini na tano (2.65) dirisha la kwanza ambalo ni la Shekh Mufidi lina upana wa mita tatu na sentimita thelathini na mbili (3.32) na la pili linaupana wa mita tatu na sentimita arubaini na mbili (3.42), katika utengenezaji wa madirisha hayo yametumika madini ya aina mbalimbali, kama vile, dhahabu, fedha, barasi, stanles, steel pamoja na mbao”.

Akabainisha kua: “Kila dirisha lina sehemu mbili, zinazo tenganishwa na sehemu ya tatu yenye mlango, kila dirisha limezungushiwa mapambo ya fedha, na kuna maandishi kwa juu, ambayo yapo ndani ya maandishi mengine yenye nakshi za mimea, pia kuna maandishi mengine juu yake yaliyo tiwa dhahabu, kila dirisha lina nguzo nne zilizo nakshiwa vizuri na zina mapambo ya mimea yaliyo tiwa fedha, vitu vyote hivyo vimebandikwa kwenye umbo la mbao za Saaji zenye uimara na ubora wa hali ya juu”.

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa kwa kiwanda cha Saqaa cha kutengeneza madirisha na milango ya makaburi na mazaru ni kukidhi haja ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na Ataba zingine na mazaru tukufu za hapa Iraq katika sekta ya utengenezaji wa madirisha ya makaburi na milango yake maalumu, pia kwa ajili ya kufanya kazi zinazo husisha dhahabu, kiwanda hiki kina vifaa vya kisasa, na kina sehemu nyingi, kila sehemu inahusika na vitu maalumu, kinaendeshwa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: