Mafundi na wahandisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na kazi ya kuweka vifuniko kwenye kubba la Masjid Sahla na katibu mkuu apongeza utendaji wa kazi…

Maoni katika picha
Bado mafundi na wahandisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha miradi wanaendelea na kazi ya kuweka vifuniko kwenye kubba la Maqaamu Swahibu Zamaan (a.f) katika Masjid Sahla, kazi inaendelea vizuri kama ilivyo pangwa na ndani ya muda tarajiwa, kubba hilo linajengwa kwa viwango bora kabisa vinavyo endana na maendeleo ya ujenzi ya sasa katika ulimwengu wa kiislamu, pamoja na kuzingatia kwa hali ya juu alama za kihistoria zilizo kuwepo na kuzirudishia kwa namna bora zaidi.

Sehemu kubwa ya ufunikaji kwa kutumia vifuniko vilivyo tiwa dhahabu imekamilika, tambua kua sehemu inayo wekwa aina hiyo ya vifuniko ni mita za mraba (80) na itatumia kiasi cha dhahabu (kilo 21), na sehemu iliyo baki itafunikwa kwa kashi Karbalai iliyo tiwa dhahabu (%30), katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (200).

Kazi ya uwekaji wa vifuniko hivyo inafanywa kwa utaalamu wa hali ya juu, kiasi kwamba vifuniko vya dhahabu na vya kashi Karbalai vinashikana vizuri na vunakua imara sana sambamba na kushikana pamoja na kubba, vinakua kama kitu kimoja kilicho kaa muda mrefu, njia hiyo ndiyo hutumiwa na mafundi pamoja na wahandisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika utendaji wa miradi ya aina hii ndani na nje ya Ataba tukufu.

Katibu wa Masjid Sahla Dokta Muhandisi Sayyid Ali Khaan Almadani amepongeza utendaji wa kazi hii, “Kutokana na umakini wa hali ya juu katika ujenzi wa kubba hii na kubakisha alama za kihistoria, jambo ambalo limefanywa kwa umaridadi mkubwa na mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kua uongozi mkuu wa Masjid Sahla ulikabidhi kazi ya kusanifu na kufunika kubba la Maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f) kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na uwezo walio nao katika utendaji wa kazi hiyo kupitia mafundi wazalendo wa Iraq, kazi kama hizo zilikua zinafanywa na makampuni kutoka nje ya Iraq, Atabatu Abbasiyya imefanikiwa kuanzisha kiwanda kinacho fanya kazi hizo kwa kiwango bora kabisa, kina uwezo wa kufanya kazi mbalimbali za kutumia dhahabu, wanaweza kuchanganya mina ya moto na ya baridi, kutengeneza madirisha ya kuweka juu ya makaburi matukufu na vinginevyo vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: