Baada ya kumaliza kuweka marumaru ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imeanza kazi ya kuweka marumaru katika uwanja wa haram yake tukufu, mafundi na wahandisi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi pamoja na wa kitengo cha wahandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza hatua ya kwanza ya kazi hiyo, ambayo imejumuisha uwekaji wa vigae vya fahari katika eneo la jengo na Kashi Karbalai.
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi hii ni miongoni mwa mradi wa uwekaji wa marumaru katika haram tukufu na kwenye uwanja wa haram katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi imegawanywa katika hatua tofauti ili isiathiri harakazi za mazuwaru au kuwazuwia, tena kila sehemu imepangiwa muda maalumu, uwanja wa haram umegawanywa vipande vipande, baada ya kumaliza kipande kimoja ndipo tunahamia katika kipande kingine kutokana na kila hatua ya kazi, hatua ya kwanza imehusisha uwekaji wa marumaru katika kuta”.
Akabainisha kua: “Marumaru mpya zitakazo wekwa ni aina ya (Malt ankos) ambazo zimefanyiwa uchunguzi wa kina kuhusu uimara wake na umadhubuti wa rangi yake, pamoja na sifa zingine ambazo ni sababu ya marimaru hizi kua bora zaidi, ukiongeza na mapambo yaliyopo katika pande zote mbili za kila jengo, zikigawanywa na sehemu ya kunywea maji ambayo imebeba tenki la maji lililopo hivi sasa”.
Akaendelea kusema: “Kazi hii ilitanguliwa na kazi zingine, ikiwemo kuondoa marumaru za zamani na gundi zake pamoja na kukarabati kuta kwa kutumia vifaa maalumu, kuhusu ujenzi wa uwanja wa haram tukufu, tayali kazi zote za chini zimesha kamilika, ikiwa ni pamoja na mtandao wa kusambaza maji, mtandao wa njia za umeme, mtandao wa kamera na mingineyo, kazi hizo zilifanywa na mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi”.
Kumbuka kua haram na uwanja wa eneo la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia miradi mingi, iliyo fanywa kwa nyakati na sehemu tofauti kutokana na aina ya mradi, orodha ya miradi hiyo inakamilishwa na mradi huu wa kuweka marumaru katika haram na uwanja wake mtukufu, kwa mara ya mwisho mradi wa aina hii ilikua katika miaka ya sabini karne iliyo pita.