Atabatu Kadhimiyya tukufu yazindua madirisha mawili la kaburi la Shekh Mufiid na Ustadhi wake ibun Quluyah na la Khawaja Nasrudini Tusi…

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza kutengenezwa katika kiwanda cha Saqaa cha utengenezaji wa madirisha na milango ya malalo matakatifu ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kumaliza kuyafunga, pia kufuatia kumbukumbu ya Idi kubwa ya Mwenyezi Mungu Idi Ghadiir, Atabatu Kadhimiyya tukufu imezindua madirisha mawili mapya la Shekh Mufiid na Ustadh wake ibun Quluyah na la Khawaja Nasrudini Tusi, mbele ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya pamoja na katibu mkuu wake Sayyid Muhammad Ashiqar na muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu wa mji wa Kadhimiyya Mheshimiwa Shekh Hussein Aali Yaasin, na muwakilishi wa Ataba tukufu na mazaru takatifu pamoja na viongozi wa dini, jamii na serikali, kwenye hafla iliyo fanyika ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Kadhimiyya bila kuwasahau watumishi wa Ataba hiyo na mazuwaru wa Maimamu wawili watakasifu Aljawadaini (a.s).

Madirisha hayo yametengenezwa katika kiwanda cha Saqaa, ambacho ni kiwanda maalumu kwa ajili ya kutengeneza madilisha na milango ya malalo matukufu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, yamepambwa vizuri na kuwekwa nakshi za kiislamu zinazo endana na muonekano mzuri wa jengo hili tukufu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an, kisha ukafuata ujumbe wa Atabatu Kadhimiyya ulio zungumzia tukio la Ghadiir, na uliwasilishwa na katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya Dokta Jamali Abdurasuul Dabbaagh, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika ukiangalia kwa makini tukio la Ghadiir utaona kua ni dahari katika siku, na sio siku katika dahari, atakaye fahamu na akatambua haki yake atafuzu duniani na akhera, na ambaye hatafahamu ataangamia duniani na akhera. Hakika Dini ilikamilishwa katika tukio la Ghadiir, kwa hiyo Ghadiir ni kilele cha ukamilifu cha umma huu, na pigo kubwa kwa washirikina na makafiri na kila anaye kubaliana nao, wakati huohuo tukio hilo linaondoa samahani kwa wale wanao potosha ukweli”.

Akabainisha kua: “Hakika Kiongozi wa Waumini (a.s) ndio sababu ya kupatikana kwa tukio la Ghadiir, kutokana na nafasi yake ndio sababu ya kuteuliwa na Mwenyezi Mungu kua kiongozi wa umma huu baada ya Mtume (s.a.w.w)”.

Akaongeza kusema kua: “Sisi tunasherehekea siku hii tukufu tukiwa na furaha kubwa zaidi kwa kuzindua madirisha mawili matukufu, la kwanza: la Shekh Mufiid na ustadhi wake ibun Quluyah (r.a) na la pili: la Shekh Khawaja Nasrudini Tusi (r.a), hakika yanastahiki kupambwa makaburi yao na kuingiza furaha katika nyoyo za waumini, yametengenezwa kwa gharama za Ataba tukufu katika kiwanda cha Saqaa kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Baada yake akapanda jukwaa Mheshimiwa Shekh Adi Alkadhimiy na akatoa muhadhara wa kidini kutokana na tukio la Ghadiir, akafafanua aya isemayo: (Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu) akaelezea yaliyo tokea baada ya amri hiyo tukufu ya kubainisha cheo cha Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), na ahadi ya Mwenyezi Mugu kwa wanadamu wote kupitia wale alio wakusanya katika eneo la Ghadiir Ghum.

Akasema kua; ahadi hii ya Mwenyezi Mungu ni tukufu sana, kila muislamu anatakiwa aiheshimu na kuilinda.

Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Kadhimiyya Mheshimiwa Shekh Hussein Aali Yaasin pia alizungumza kuhusiana na tukio hilo, akasema kua: “Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye amerahisisha na anawarahisishia waumini kutambua imani yao na kutekeleza ibada zao na maadhimisho yao, na anawawezesha kujenga nyumba ambazo ameamrisha zinyanyuliwe na kutajwa nadi ya nyumba hizo jina lake, tuna muomba Mwenyezi Mungu auwezeshe mkusanyiko huu kuhuisha mambo yake”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika madirisha haya mawili yametengenezwa na raia wa Iraq, hii ni neema miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kwetu, bila shaka mnatambua tofauti kubwa aliyo kuwa nayo Mtume (s.a.w.w) inatokana na elimu yake na uwezo mkubwa wa akili yake na utakasifu wake, mambo amabyo alimfundisha Ali (a.s) na yakamfanya awe Imamu na atukuzwe, kutokana na utukufu wa elimu leo hii tunamtukuza Shekh Mufiid na wanachuoni wetu wacha Mungu, hakika wanachuoni wetu wanaolinda Dini na kufanya kazi kwa ajili ya akhera yao, na kujitenga na machafu ya Duniani, yatupasa kushikamana nao pamoja na kushikamana na vizito viwili tukiwa na imazi thabiti, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuthibitishe katika haki kwa sababu Ali yupo pamoja na haki na haki ipo pamoja na Ali”.

Naye msomaji wa mashairi ambaye ni mtumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) bwana Ali Swafaar Alkarbalai akasoma kaswida isemayo (Uzuri wa Ghadiir) iliyo burudisha wahudhuriaji. Aidha hafla ilipambwa na mashairi kutoka kwa mtumishi wa Maimamu wawili Aljawadaini (a.s) bwana Husseini Karaar Alkadhimiy ambayo yaliwaburudisha wahudhuriaji na mazuwaru watukufu.

Hafla ikahitimishwa na tukio la kukabidhi funguo za madilisha mawili mapya, dirisha la kaburi la Shekh Mufiid na Ustadh wake ibun Quluyah, na dirisha la Khawaja Nasrudini Tusi (r.a) kutoka kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhammad Ashiqar ambaye alimkabidhi funguo hizo katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya tukufu Dokta Jamali Abdurasuul Dabbaagh.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: