Baara ya kusimama kazi zaidi ya mwezi kwa sababu ya ziara ya Arubaini, leo mafundi wanaendelea na hatua ya pili ya mradi wa kufunika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inayo husisha sakafu na eneo la katikati baina ya sakafu na kashi Karbalai.
Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, akaongeza kua: “Kwa baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu tumeanza hatua ya pili ya sehemu ya pili ya mradi huu, baada ya kumaliza sehemu ya kwanza ambayo ilihusisha eneo la baina ya mlango wa Alqamiy na Imamu Ali Haadi (a.s), iliyo kamilika kabla ya ziara ya Ashura na Arubaini, kwa ajili ya kutoa nafasi kwa mazuwaru na kuto katisha katisha kazi kwa sababu ya kuwapisha mazuwaru tulisimamisha kazi, leo tumeanza tena kazi, katika awamu hii tunafanya matengenezo katika eneo lililopo baina ya milango miwili, mlango wa mkono (kafu) na Alqamiy kusini mashariki ya Ataba ambako kuna maeneo tisa”.
Akabainisha kua: “Kazi hii imetanguliwa na maandalizi kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuondoa madini sambamba na marumaru za zamani na kukarabati ukuta na sakafu pamoja na kuziba sehemu zilizo pasuka, halafu tumeweka vipande vingine kwa ajili ya kuweka marumaru juu yake, na tumeweka mtandao wa umeme, mawasiliano na mengineyo”.
Kuhusu wasifu wa marumaru zinazo wekwa amesema kua: “Marumaru mpya zinazo weka ni za aina ya (Malt oncsi), zimetengenezwa kwa kiwango maalumu kinacho endana na sehemu zinapo wekwa sawa iwe kwenye sakafu au ukutani, zimefanyiwa majaribio mara kadhaa kuhusu uimara na rangi yake, pamoja na sifa zingine nyingi zinazo zifanya marumaru hizi kua bora zaidi, ukiongeza na uzuri wa mapambo yaliyopo katika marumaru hizo”.
Kumbuka kua haram na uwanja wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia utekelezwaji wa miradi mingi kwa muda na sehemu maalumu, mfululizo wa miradi hiyo unahitimishwa na mradi muhimu kama iliyo tangulia, ambao ni ufunikaji (uwekaji marumaru) wa haram na uwanja wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kazi iliyo fanywa miaka ya sabini karne iliyo pita kwa mara ya mwisho.