Miongoni mwa uboreshaji wa kisasa uliofanywa na mafundi wa kiiraq katika mradi wa upanuzi wa maqamu ya Inanmu Mahdi (a.f)…

Maoni katika picha
Juhudi kubwa inayo fanyika itokanayo na mwenye maqamu takatifu, kazi ya upanuzi wa maqamu ya Imamu Mahdi (a.f) inaendelea na imepiga hatua kubwa, tayali uzuri wake umeanza kuonekana bayana, kazi hiyo imefanywa na mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaofanya kazi katika kitengo cha miradi ya kihandisi, wamesimama imara kutekeleza mradi huu chini ya usanifu wa kisasa na kufanya kazi kwa ufanisi na ubora katika kila hatua, kwa kiansi ambacho ujenzi huu unafanana na ujenzi uliofanyika katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuendana na utukufu wa eneo hili kwa mazuwaru wanaokuja kufanya ziara.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ametuambia kazi zilizo kamilika katika mradi huu kua: “Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za mwenye maqamu hii takatifu na juhudi za wafanyakazi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) hawaja simama au hata kuzembea katika kazi, kazi inafanyika kama ilivyo pangwa, ujenzi wa eneo lililo ongezwa katika maqamu lenye ukubwa wa mita za mraba zaidi ya (1000) umekamilika, eneo hilo linajumuisha ukumbi wa wanawake wenye ukubwa wa mita za mraba (490) na ukumbi wa wanaume wenye ukubwa wa mita za mraba (310), na ukumbi mwingine wa watumishi wenye ukubwa wa mita za mraba (150), kazi ya kufanya marekebisho ya kumalizia imeanza upande wa ndani na nje pamoja na kuweka nakshi na mapambo ya ukutani, kazi hii imepiga hatua kubwa sambamba na ufungaji wa umeme na sistim ya spika pamoja na vitu vingine vinavyo fanywa pamoja na mradi huu.

Akaongeza kua: “hali kadhalika imeanza kazi ya kuongeza eneo lingine upande wa mbele litakalo tumika kama sehemu ya kuingilia, eneo hilo litakua na mlango mkubwa utakao wekwa ulipokua mlango wa zamani, ukifuatia na sehemu yenye upana wa mita nne na pembezoni mwake kutakua na nguzo zitakazo wekwa nakshi za Kashi Karbalai, ujenzi huu umetumia vyuma nao ni ujenzi mpya katika mradi”.

Kumbuka kua maqamu ya Imamu Mahdi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya wa sasa katika lango la Karbala kwenye njia inayo elekea katika maqamu ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) nayo ni mazaru mashuhuri, Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya matengenezo katika maqamu hiyo kuanzia kwenye kubba hadi katika kumbi za haram na sehemu zingine za maqamu hii, kwa kua sehemu ilipo maqamu haiwezi kufanyiwa upanuzi kupitia pande zake tatu, imebidi upanuzi ufanyike upande wa mto wa Husseiniyya ambao ni upande wa magharibi, tena kwa kutumia nguzo na kujengwa kwa muundo wa daraja bila kufunga hata kidogo njia ya maji, eneo lililo ongezwa linakaribia mita za mraba (1200) na unaweza kuingia katika maqamu kwa kutumia njia na milango maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: