Kukamilika kwa kazi ya kuweka daraja katika maqaamu ya Imamu Mahdi (a.f)…

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wamekamilisha sehemu moja ya kazi ya upanuzi wa maqamu ya Imamu Mahdi (a.f) inayo fanywa na kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi huo umesha piga hatua kubwa, tayali daraja linalo unganisha pande mbili za mto huo limesha wekwa zege na kuanza kutumiwa na mazuwaru ambao wamepongeza sana ujenzi wa daraja hilo kwani limepunguza msongamano.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh: “Mradi huu unatekelezwa chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa kitengo cha miradi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ujenzi unaofanyika unaubora wa hali ya juu, baada ya kuweka zege katika nguzo na pembezoni mwa daraja wamemalizia kwa kumwaga zege katika daraja lenyewe na kukamilisha ujenzi huo”.

Akaongeza kua: “Daraja linaupana wa mita (7) na urefu wa mita (22), daraja hili limekua msaada mkubwa kwa daraja lililo kuwepo na limesaidia kupunguza msongamano wa mazuwaru”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo maqamu hii ipo chini yake, iliyopo kushoto mwa mto Husseiniyya unapo ingia katika mji wa Karbala, ilichukua jukumu la kuikarabati na kuifanyia upanuzi na ikaweka mkakati wa utekelezaji, miongoni mwa kazi zilizo fanyika hivi karibuni katika mradi wa upanuzi ni ujenzi wa daraja la pili linalo unganisha pande mbili za mto huo, na kua msaada mkubwa kwa daraja lililo kuwope, kutokana na msongamano mkubwa uliokua unashuhudiwa kwenye daraja hilo hasa katika siku za ziara maalumu, mbali na udogo wake pamoja na ukongwe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: