Akaongeza kua: “Hatua ya kuweka maandishi ya Qur’ani ni miongoni mwa hatua muhimu katika mradi huu, mafundi wametumia nguvu zao zote kuhakikisha wanakamilisha hatua hii pamoja na hatua zingine za mradi huu, kazi ya kuweka herufi ni sawa na kazi ya kupamba, kwani inapendezesha ukuta tena kwa herufi tukufu zilizo pambwa na zenye rangi ya kupendeza, kwa kupendezesha zaidi hati zimenakshiwa kwa mapambo ya kiislamu yanayo endana na utukufu wa eneo hili”.
Kumbuka kua herufi hizo ni za aya za Qur’ani tukufu na zimewekwa sehemu tatu, ili zaairu aweze kuzisoma kwa ukamilifu, wasifu wa herufi hizo upo kama ifuatavyo:
- - Aina ya hati ni Thuluth Jalliy iliyo shiba na kutiwa dhahabu Ayari (24) yenye viwango vitatu na ubapa wa jino la kalam (sm3.6), kazi hii imefanywa na mchoraji wa kiiraq anaeitwa Ustadh Farasi Abbasi.
- - Ubavu wa kulia unakipimo cha (sm70 x sm351) zilizo andikwa surat Ikhlasi.
- - Upande wa katikati mbele ya Twarima unakipimo cha (sm70 x sm700) zimeandikwa sehemu ya aya ya (177) katika surat Baqarah.
- - Upande wa kushoto unakipimo cha (sm70 x sm 349) na zimeandikwa surat Kauthar (Innaa a’twainaakal kauthar…).
- - Jumla ya pande zote tatu inakua ni (m14 x sm70).
- - Vipande vya maandishi vimetiwa dhahabu halisi na kuvishwa Mina ya bluu.
- - Maandishi yanamapambo mazuri ya kiislamu upande wa juu (sm 20) na upande wa chini kiwango hicho hicho, na vimetiwa dhahabu ya ujazo wa Ayari (24).