Kwa picha: Ujenzi wa majengo ya chuo kikuu cha Alkafeel katika mji wa Najafu uanaendelea vizuri

Maoni katika picha
Hatua kubwa imepigwa katika ujenzi wa majengo ya chuo kikuu cha Alkafeel mkoani Najafu, chini ya mkakati maalumu, na kwa ajili ya kukamilisha hatua za ujenzi moja baada ya nyingine, hatua ya kwanza inaendelea vizuri na mafanikio yake yanaonekana wazi, inatokana na juhudi za watendaji wa shirika waliokabidhiwa jukumu hilo pamoja na juhudi zinazo fanywa na wataalamu wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi, pamoja na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ametuambia kuhusu ujenzi huu kua: “Ujenzi unaendelea katika chuo kikuu cha Alkafeel, hatua ya kwanza vinajengwa vitivo vitatu, ambavyo ni: (Famasiya, udaktari wa meno na kompyuta), katika eneo linalo kadiriwa kufika mita za mraba (1500) kila kitivo kitakua na jengo la ghorofa nne, pamoja na kuzingatia maelekezo ya wizara ya elimu ya juu ya Iraq yanayo husu ujenzi wa vyuo vikuu binafsi, vitivo hivyo vinajengewa mahitaji yote ya kimasomo na kiutawala, kwa kufuata mchoro ulioandaliwa wa kila kitivo, kuanzia kumbi za madarasa, maabara, maktaba, kumbi za mikutano, vyumba vya ofisi na mengineyo, ujenzi unafanyika kisasa pia kuna sistim ya mawasiliano na kamera, pia kuna eneo kubwa la bustani na barabara pamoja na sehemu ya kuegesha magari, tunamshukuru Mwenyezi Mungu ujenzi wa kitivo cha Famasiya umekamilika kwa asilimia (%80), na kitivo cha udaktari wa meno asilimia (%60) na kitivo cha kompyuta asilimia (%40), tunatarajia kukamiliza ujenzi huu mwanzoni mwa mwaka ujao –Insha-Allah- majengo hayo yataanza kutumika baada ya likizo ya nusu mwaka”.

Akasisitiza kua: “Hakika majengo yote ya chuo na yale yanayo fungamana nayo yanajengwa kwa viwango tulivyo kubaliana na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu”.

Akasema kua: “Mradi huu utafanya mambo mengi miongoni mwa mambo hayo ni:

  • - Kulea vipaji vya wairaq na kunufaika navyo.
  • - Kuandaa mazingira rafiki ya kujisomea yanayo kidhi vigezo vya elimu vya kimataifa.
  • - Kutoa fursa za kazi kutokana na uwezo wa majengo hayo.
  • - Kupunguza msongamano uliopo katika vyuo binafsi na vya serikali.
  • - Kwenda sambamba na maendeleo ya kielimu katika sekta ya nadhariya na vitendo, kwa mujibu wa selebasi.

Kumbuka kua ujenzi huu ni miongoni mwa mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu unaolenga kuboresha sekta ya elimu hapa Iraq, na kwenda sambamba na maendeleo ya Dunia, baada ya kukamilisha hatua za uanzishaji wa taasisi za elimu na malezi sasa hivu tumeingia katika hatua ya kujenga majengo ya taasisi hizo, na jambo muhimu zaidi ni kua na majengo yanayo endana na mazingira ya taasisi hizo na majengo haya ni moja ya utekelezaji wa jambo hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: