Ardhi imeandaliwa kisasa na watumishi wa vitalu vya Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao wanauzowefu mkubwa unao wawezesha kufanya miradi kama hii.
Mtandao wa kimataifa Alkafeel umeongea na rais wa kitengo cha utumishi na msimamizi mkuu wa mradi huu bwana Khaliil Hanuun ambaye amesema kua: “Shamba la mfano la kunazi limeanza kuandaliwa baada ya mafanikio yaliyo patikana katika shamba la mfano la tende, pia ni sehemu ya fikra na maoni yaliyo tolewa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, tumefanyia kazi fikra na maoni hayo na kutekeleza kwa vitendo, ndipo tulipo anzisha shamba la kilimo hiki ambacho kinafanyika kwa mara ya kwanza hapa Iraq, tena tumepanda aina adimu zaidi ya kunazi, katika eneo linalo milikiwa na Atababatu Abbasiyya tukufu kwenye barabara ya (Najafu – Karbala), tunategemea kuziba pengo la mahitaji ya zao hili ambalo hutumika kwa chakula na tiba hapa nchini, vilevile mradi huu utachangia kuongeza eneo la kijani kibichi katika mkoa wa Karbala na kunufaika na jangwa lake, pia mradi huu unatupa uzowefu wa kufanya miradi mingine inayo fanana na huu, tunatarajia kufanya miradi mingine kama vile kilimo cha komamanga na tini”.
Mtaalamu wa kilimo bwana Mu-ayyad Haatif ambaye ni kiongozi wa vitalu vya Alkafeel amesema kua: “Shamba la kunazi ni moja ya mashamba ya mfano ya mazao yatakayo limwa baadae, limelimwa katika eneo lenye ukubwa wa Dunam (70) tumeligawa sehemu tano, kila sehemu inaukubwa wa Dunam (15) takriban, kazi hiyo ilitanguliwa na kazi za utangulizi zifuatazo:
- - Kuchunguza aina ya udongo na kufanya uchambuzi wa kawaida wa udongo na maji, kwa ajili ya kubaini kiwango cha chunvi na kuchagua njia bora ya kunufaika na ardhi hiyo katika kilimo, uchunguzi wote ulifanywa na wataalamu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Kufanya upembuzi yakinifu wa shamba na kubaini sehemu za kupanda miti ya kunazi.
- - Kufanya kazi ya kusawazisha ardhi katika kila sehemu ya shamba.
- - Kuainisha sehemu za kupanda miti.
- - Kufunga mtandao mpya na wa kisasa wa kumwagilizia miti kwa kutumia maji ya ndani.
- - Kuweka mbolea ya samadi katika ardhi kwa ajili ya kuirutubisha na kufanya miti iote kwa haraka.
Akaongeza kua: “Hatua ya kwanza tumepanda miti (1900), baada ya kufanya majaribio ndani ya nje ya Iraq, aina hii ni bora zaidi kama vile aina za Epo, Zaituni, Armutwi na zinginezo, pia miti hii inasaidia kuzuwia upepo mkali wa jangwani”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imesha tekeleza miradi mingi ya kilimo, na inalipa umuhimu zaidi swala la kilimo, kwani ni moja ya sekta muhimu za uchumi hapa nchini, inafanya kila njia kutekeleza miradi ya kilimo.