Mradi wa jengo la vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu upo katika hatua za mwisho na kazi inaendelea vizuri…

Maoni katika picha
Mradi wa jengo la vitengo vya Atabatu Abbasiyya ni miongoni mwa miradi muhimu inayo fanywa na Ataba tukufu, baada ya kukamilika jengo hilo ofisi nyingi za vitengo zilizopo ndani ya jengo tukufu la Ataba zitahamishiwa katika jengo hilo, jengo hilo linaukubwa wa mita za mraba (1500), lina ghorofa (12), kila ghorofa litatengewa kitengo kimoja miongoni mwa vinengo vya Ataba au vitengo viwili kutokana na ukubwa wa mahitaji ya kitengo, jengo la chini ya usawa wa ardhi linaukubwa wa mita za mraba (1100), litatumika kama sehemu ya kuegesha magari, ghorofa la chini litatumika kwa ofisi za mapokezi pamoja na chumba cha wahudumu, ghorofa zilizo baki zitatumika kama ofisi za vitengo vya Ataba, kila ghorofa linaukubwa wa mita za mraba (1250).

Kuhusu maendeleo ya kazi katika mradi huu tumeongea na Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu amesema kua: “Mradi unaendelea vizuri tunatarajia kuukamilisha ndani ya muda uliopangwa, ujenzi wa boma upo hatua za mwisho, kiwango cha ukamilifu kinakaribia asilimia %90, sambamba na kazi hii kuna kazi zingine zinaendelea, kama vile kazi ya kukata vyumba, kufunga nyaya za umeme, kuweka mtandao wa zima moto, mtandao wa sauti (spika), mtandao wa mawasiliano na zinginezo, pamoja na kuweka mfumo wa viyoyozi”.

Akaongeza kua: “Kitengo kimewafanyia wepesi katika kila jambo watekelezaji wa mradi huu ambao ni shirika la biashara na ujenzi Twayyibah, nalo linatumia nguvu zake zote kwa ajili ya kushinda kila aina ya kikwazo, kiwango cha kukamilika mradi kimefika hatua kubwa na kazi inaendelea vizuri”.

Kumbuka kua ujenzi wa mradi huu umetokana na maendeleo makubwa yanayo shuhudiwa katika vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani asilimia kubwa ya vitengo hivyo, ofisi zao zipo ndani ya jengo la haram tukufu, kwa ajili ya kutoa nafasi kwa mazuwaru na kuifanya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ipo kwa ajili ya kufanya ziara na ibada peke yake, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umeamua kujenga jengo maalumu litakalo beba vitengo vyote vya Ataba na idara zake, hivyo vitengo vyote vitakua katika jengo moja chini ya utaratibu wa taasisi wa kisasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: