Baada ya kumaliza ujenzi wa majengo ya chini: imeanza kazi ya kuweka lami katika barabara za mradi wa maegesho ya Alkafeel

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza ujenzi wa chini katika mradi wa maegesho ya Alkafeel pamoja na ujenzi wa maeneo yake yote matano, imeanza kazi ya kuweka lami katika barabara kuu na ndogo, kwa kufuata viwango vilivyo pangwa vinavyo endana na matumizi ya barabara hizo.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhwiyaau Majidi Swaaigh ameueleza mtandao wa Alkafeel kua: “Mradi wa maegesho ya Alkafeel unachukuliwa kua mradi mkubwa na wa kimkakati unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi wowote wa aina hii hupata changamoto za kuchelewa baadhi ya mambo katika utekelezwaji wake, mara nyingi changamoto hizo zinakua nje ya uwezo wetu na uwezo wa mashirika mawili yanayo tekeleza mradi –Shirika la ardhi tukufu na shirika la uchumi Alkafeel- mashirika hayo yanafanya kila yawezalo kuhakikisha yanamaliza kazi kwa muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kazi inaendelea vizuri, anaye kwenda Najafu kutokea Karbala tukufu bila shaka ataona maendeleo ya mradi huu unao tekelezwa kwa umakini”.

Akaongeza kua: “Leo hii tumefika katika hatua muhimu ya kukamilisha mradi ambayo ni hatua ya kuweka lami baada ya kumaliza ujenzi wa chini, uliohusisha kujenga mtandao wa maji ya mvua, umeme na mingine, lami inawekwa kisasa zaidi kwa kutumia mtambo wa kisasa wa kuchanganyia, unao endana na ukubwa wa mradi, chini ya makubaliano maalumu ya hatua zote tano za mradi na uwekaji lami katika barabara kubwa na ndogo”.

Akabainisha kua: “Hakika kazi ya kuweka lami imepitia hatua nyingi miongoni mwa hatua hizo ni:

  • - Kukamilisha uwekaji wa lami katika njia.
  • - Kufanya upembuzi yakinifu kwa kila njia kwa ajili ya kubaini ujazo wa lami unao takiwa kutokana na mwinuko na mabonde yake.
  • - Kuweka tabaka la udongo safi utakao hifadhi mabomba yanayo pita chini.
  • - Kuweka tabaka la lami peke yake.
  • - Kusawazisha njia zote pamona na kurekebisha sehemu mbovu.
  • - Kuweka tabaka tofauti za kifusi.
  • - Kumwagilia maji na kushindilia.
  • - Kusawazisha tabaka la juu linalo beba lami.
  • - Kuweka tabaka la lami nyepesi.
  • - Kusawazisha tena kwa mara ya mwisho.
  • - Kufanya tathmini ya mwisho kwa ajili ya kubaini viwango”.

Akaendelea kusema: “Kazi inaendelea vizuri katika mazingira salama na inatarajiwa kukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa”.

Kumbuka kua maegesho ya Alkafeel ni maegesho ya kwanza kujengwa kwa mtindo huu ambao umekidhi viwango vya kimataifa, yanajengwa katika eneo lenye ukubwa wa (72.125 m2) ukubwa wa jengo ni (42.000 m2) limegawanywa sehemu tano ambazo ni:

  • 1- Jengo la utawala.
  • 2- Jengo la kituo cha mafuta.
  • 3- Jengo la gereji ya magari madogo.
  • 4- Jengo la gereji ya magari makubwa.
  • 5- Jengo la kuegesha magari (madogo na makubwa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: