Kiwango cha ukamilifu katika mradi wa kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ametaja kiwango cha ukamilifu katika mradi wa jengo la kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati linalo jengwa katika mkoa wa Najafu Ashrafu, jengo hilo limekamilika kwa asilimia (%87), hivi sasa wanaendelea na kazi za kumalizia (finishing) na tunaona limekidhi vigezo vilivyo pangwa. Limejengwa kisasa na kwa umaridadi wa hali ya juu.

Akaongeza kua: “Mradi huu unajengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (890) jengo lina ghorofa saba, limefanyiwa usanifu maalumu katika ujenzi na umaliziaji unao endana na makusudio yake, ili liwe jengo la kupigiwa mfano katika mji wa kiongozi wa waumini (a.s) lenye utukufu wa Abbasiyya”.

Akasema kua: “Manbo yaliyo kamilika katika kazi iliyo fanywa tunaweza kuyataja kwa ufupi kua ni:

  • - Kukamilika kwa ujenzi wa boma la jengo.
  • - Kukamilika ukataji wa nyumba katika kila ghorofa.
  • - Kukamilika kwa mtandao wa kusambaza maji.
  • - Kukamilika kwa ufungaji wa nyaya za umeme, kwa kufuta ramani iliyo andaliwa pamoja na hakiba ya upanuzi wa baadae.
  • - Kukamilika kwa kazi ya uwekaji wa milango na madirisha.
  • - Kukamilika kwa uwekaji wa paa la pili (jipsam bord na vipande vya madini) katika ghorofa zote.
  • - Tumefika Asilimia (%85) ya upakaji wa rangi ndani na nje ya jengo.
  • - Kukamilika kwa upigaji wa plasta (ripu) yenye muonekano wa kisasa na kizamani pamoja na kuweka (curtain wall).
  • - Ufungaji wa ngazi (lifti za umeme) zipatazo nne umekamilika kwa asilimia (%80).
  • - Kukamilika kwa mitandao ya utowaji wa huduma (mtandao wa kutoa wito, zima moto, kamera, mawasiliano na mtandao wa gesi)”.

Kumbuka kua mradi huu unajengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (890) jengo lina ghorofa saba, limefanyiwa usanifu maalumu katika ujenzi na umaliziaji unao endana na makusudio ya kituo pamoja na matarajio ya sasa na baadae, fahamu kua kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimesha fanya makumi ya miradi mikubwa pamoja na mamia ya miradi midogo na ya kati (ukiwemo mradi huu), miradi hiyo imefanywa ndani na nje ya Ataba tangu kuanzishwa kwake baada ya uanguka utawala wa kidikteta uliopita, asilimia kubwa ya miradi hiyo imefanywa na raia wa Iraq, na iliyo fanywa na watalamu wa kigeni ni michache sana.

Fahamu kua kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ambacho makao makuu yake yapo Najafu Ashrafu ni miongoni mwa vituo muhimu, kutokana na ukubwa wa kazi zake na wingi wa idara zake (ambazo ni sita) pamoja na matawi yake, sehemu ilipo kwa sasa haiendani na huduma inazo toa pamoja na maendeleo yake, na kwa upande mwingine hapaendani na mahitaji ya sasa wala ya baadae, ndipo Atabatu Abbasiyya ikaamua kujenga jengo maalumu kwa ajili ya kituo hicho. Kwa maelezo zaidi tembelea toghuti ifuatayo: https://www.iicss.iq/ .
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: