Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu atembelea mradi wa chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) ametembelea mradi wa chuo kikuu cha Alkafeel ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya mkoa wa Najafu Ashrafu, akiwa na jopo la viongozi likiongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhammad Ashiqar (d.t) pamoja na wajumbe wa kamati yake ya uongozi na marais wa vitengo vya Ataba, sambamba na Masayyid na wakuu wa vitengo katika chuo hicho.

Ziara hii ni kwa ajili ya kuangalia ulipo fika mradi kwa ujumla na kwa namna ya pekee mradi wa kitivo cha famasia, kama sehemu ya maandalizi ya ufunguzi wake na kuhamisha wanafunzi pamoja na wakufunzi kutoka katika jengo la zamani na kuwaleta kwenye jengo jipya, katika msimu wa pili wa mwaka huu wa masomo, Mheshimiwa ametembelea sehemu tofauti za chuo na kuangalia vifaa vya kisasa vilivyopo,

Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) amesema kua: “Atabatu Abbasiyya daima inapambana kuboresha sekta ya elimu, ikiwemo elimu za sekula na hili ndio lililotusukuma kufanya mradi huu, tunaamini kua wataalamu watafanya kila wawezale kuboresha sekta ya elimu”.

Akaongeza kusema: “Tunamshukuru kila aliye saidia mradi huu kufika hapa pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo, ni matumaini yetu mazingira haya yatawafaa wanafunzi watakapo kuja kuendelea na muhula wa pili katika mwaka wa masomo kwenye jengo hili jipya, pia tunatarajia wafanye vizuri zaidi katika masomo yao, akasisitiza kua mwaka kesho vitafunguliwa vitivo vingine”.

Naye rais wa chuo kikuu cha Alkafeel Dokta Nuuris Dahani wakati akitoa maelezo kwa wahudhuriaji amesema kua: “Kulikua na ufatiliaji mzuri kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu kuhakikisha chuo hiki kinajengwa kwa kufuata viwango vya kimataifa sambamba na maendeleo ya ulimwengu wa sasa”.

Rais wa miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhwiyaau Majidi Swaaigh ametoa maelezo kwa ufupi kuhusu mambo muhimu waliyo fanya katika kutekeleza mradi huu, akasema kua; jengo hili lilipangwa kua la kimataifa toka katika hatua za mwanzo katika michoro na hivyo hivyo imekua katika ujenzi wake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mhandisi Farasi Abbasi Hamza kiongozi wa idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu ameelezea vitu vya kisasa vilivyo wekwa katika jengo hili, ikiwa ni pamoja na mfumo wa mawasiliano, vipaza sauti, mfumo wa kutoa tahadhari, kamera pamoja na mifumo mingine, ujenzi umefanyika kwa ubora wa hali ya juu na jengo hili linakidhi mahitaji ya wakufunzi na wanafunzi.

Fahamu kua kitivo cha famasia ni moja ya vitivo vya chuo kikuu cha Alkafeel ambacho kipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya ndani ya mkoa wa Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: