Kumaliza hatua muhimu katika mradi wa kuunganisha sardabu ya Imamu Hussein na Imamu Jawaadi (a.s) pamoja na sardabu ya eneo lililoongezwa la nje…

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wanaofanya kazi katika mradi wa kuunganisha sardabu mbili ya Imamu Hussein na Imamu Jawaadi (a.s) ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na sardabu ya eneo la nje lililo ongezwa, wamemaliza hatua muhimu tena kwa viwango vilivyo pangwa pamoja na changamoto zilizopo, wamemaliza hatua ya uchimbaji na kusawazisha ardhi pamoja na kujenga kuta na mambo mengine, kazi hizo ndio msingi muhimu wa kuelekea hatua zingine za mradi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ambaye ni rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu aliyo toa kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel, amesema kua: “Kwa baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu na mwenye malalo hii takatifu pamoja na juhudi za watumishi tumemaliza hatua muhimu za mradi huu, pamoja na mazingira yaliyo kuwepo, tumechimba kwa kiwango kikubwa chini ya moja ya milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuta za jirani yake, pamoja na kukutana na maji lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kazi imekamilika”.

Akaongeza kua: “Baada ya kumaliza kazi ya kuchimba iliyo fanywa kwa ustadi mkubwa na kwa kutumia mitambo maalum na kufuata vipimo vilivyo pangwa vinavyo endana na kiwango cha sardabu ya ukumbu wa haram tukufu pamoja na eneo lililo ongezwa, ardhi imesawazishwa kwa kutumia vifaa maalum sambamba na kuweka zege sehemu ya chini na kwenye kuta, na kujenga ukuta wa tofali za bloko zenye Sement kali na kufika katika hatua ya kuweka paa”.

Kumbuka kua mradi huu ni sehemu ya miradi ya ujenzi inayo endelea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuweka uwiyano wa jengo, hasa katika miradi ya ujenzi wa sardabu na upanuzi wa ukumbi wa haram tukufu, katika mradi huu yatafanyika mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni:

  • - Sardabu ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) itaonganika ndani na nje na kua moja.
  • - Itaondoa usumbufu kwa mazuwaru kwa kuwawezesha kutembea katika sardabu bila kupitia katika milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Kuunganisha sardabu mbili zilizopo upande wa mlango wa Imamu Hassan (a.s).
  • - Kuunganisha milango ya sardabu zote (ya uwanja wa haram na eneo lililo ongezwa) katika sehemu kuu moja.
  • - Baada ya kukamilika mradi itatengwa sehemu ya wanawake kutokana na sehemu iliyo ongezwa kwa ajili yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: