Baada ya kumaliza awamu ya tano: Utendaji wa kazi unaelekea sehemu nyingine katika mradi wa uwekaji wa marumaru katika jengo la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Utendaji wa kazi za mradi wa kuweka marumaru katika jengo la haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), unao husisha kuweka marumaru chini na matika eneo linalo tenganisha sehemu ya chini na kashi karbalai unaingia awamu ya sita, ambayo inahusisha eneo lililopo katikati ya mlango wa Kibla na Amirulmu-uminina (a.s), upande wa kusini wa haram takatifu, baada ya kumaliza kazi zote katika awamu ya tano, iliyo husisha eneo la katikati ya mlango wa Imamu Mussa bun Jafari na mlango wa Imamu Hassan (a.s), katika upande wa magharibi wa haram tukufu.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Shwaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi hizi ni miongoni mwa mradi wa kuweka marumaru katika haram takatifu na kwenye eneo lenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), kazi imepangwa kwa awamu kwa namna ambayo haizuwii harakati za mazuwaru, sambamba na kila awamu kuipangia muda maalumu, kila baada ya kumaliza awamu moja tunahamia katika awamu nyingine kwa kufuata utaratibu maalumu uliopangwa”.

Akaongeza kua: “Kazi hii haijaishia kwenye uwekaji wa marumaru peke yake, bali kuna kazi za utangulizi, kama vile kutoa marumaru za zamani na kusawazisha ukuta na sakafu kwa ajili ya kuweka marumaru mpya, sambamba na kuweka tabaka ya chuma kwa ajili ya kuwekwa marumaru juu yake, pia tunaweka nyaya za umeme na za mfumo wa vipaza sauti (spika), na kutandika mabomba ya mfumo wa maji na yote inaonganishwa na mifumo mikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kua: “Marumaru mpya zinazo wekwa ni za aina ya (Malt Oksi), zimesha fanyiwa utafiti mara nyingi wa kitalamu na kihandisi, kuhusu uimara, uhalisi na ujazo wake, hizi ndio marumaru bora zilizopo sokoni, sambamba na mapambo mazuri ziliyo nayo”.

Akasisitiza kua: “Hakika kazi inafanyika kama ilivyo pangwa na kwa ufanisi mkubwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu inatarajiwa kukamilika kwa wakati na kwa ubora mkubwa”.

Kumbuka kua haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia utendaji wa miradi mingi, iliyo pangiwa wakati na sehemu maalumu, mfululizo wa miradi hiyo unahitimishwa na mradi wenye umuhimu sawa na iliyo tangulia, mradi wa uwekaji marumaru katika jengo la haram tukufu, ambapo iliwekwa marumaru kwa mara ya mwisho katika miaka ya sabini karne iliyo pita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: