Maoni katika picha
Akaongeza kua: “Tumepiga hatua kubwa katika utendaji wetu unao kwenda sambamba na malengo yote ya mradi, miongoni mwa hatua tulizo piga ni:
- - Tumeanza kuweka maraya (marumaru za vioo) katika paa na kwenye kuta za kumbini.
- - Tunaendelea kuweka mifumo muhimu katika jengo kama vile kufunga nyaya za umeme, mfumo wa kutoa tahadhari, zima moto, mawasiliano, ulinzi na mingineyo.
- - Kazi inaendelea katika mlango mkuu wa Maqaamu ikihusisha sehemu ya mlango wa zamani kwa nje, ikifuatiwa na eneo lenye ukubwa wa mita nne na pembeni yake kuna nguzo zingine zitakazo wekwa kashi karbalai, katika kazi hii limetumika umbo la chuma ambalo ni sehemu mpya zilizo ongezwa katika mradi huu.
- - Kazi ya kuweka marumaru inaendelea katika eneo la saa kuu iliyopo juu ya Maqaamu upande wa mbele”.
Kumbuka kua Maqaamu ya Imamu Mahadi (a.f) ipo upande wa kushoto wa mto wa Husseiniyya wa sasa, unapo ingia katika mji wa Karbala kwa kupitia barabara inayo elekea katika Maqaamu ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) nayo ni mazaru mashuhuri, Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua jukumu la kuikarabati na kuifanyia upanuzi kuanzia kwenye kubba hadi katika kumbi za haram na sehemu zingine, kwa kua sehemu ilipo Maqaamu haiwezi kufanyiwa upanuzi katika pande zake tatu, upanuzi umefanywa upande wa mto wa Husseiniyya, umbao ni upande wa magharibi kwa kutumia nguzo za zege na kuweka daraja juu yake, bila kuzuwia njia ya maji au kubadilisha muelekeo wake, eneo lililo ongezwa linakadiriwa kua na ukubwa wa mita za mraba (1200) na linaungana na Maqaamu kupitia milango maalumu.