Maoni katika picha
Kuhusu mradi huu tumeongea na Mhandisi Alaa Hussein kutoka kitengo cha usimamizi wa kihandisi amesema kua: “Tumeanza kazi ya ujenzi katika hatua tofauti, tumeanza kwa kuweka nguzo kwa kutumua vifaa vya chuma vilivyo tengenezwa na kitengo cha uhandisi, baada ya kuweka nguzo tukazisakafia kwa block, halafu tukaziwekea mfumo wa umeme na mawasiliano”.
Akaongeza kua: “Muda wa kazi uliopangwa kwa kila ghorofa ni miezi mitatu, kwa kufanya kazi kila siku saa (24), idara zoto zilizo chini ya usimamizi wa kihandisi zinashiriki katika ujenzi huu, zikiongozwa na idara ya majengo ya nje”.
Fahamu kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kina nafasi kubwa katika ujenzi wa majengo mengi ambayo yapo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ndani na nje ya Ataba, kina mafundi mahiri wenye uzowefu mkubwa wa aina zote za ujenzi.