Upande wa kusini wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umewekwa marumaru mpya za kifahari.

Maoni katika picha
Upande wa kusini wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umepata muonekano mpya baada ya kuwekwa marumaru za kufahari, sehemu ya sita ya mradi wa kuweka marumaru katika kuta na ardhi, sehemu hii inaunganishwa na sehemu tano zilizo kamilika, kazi itaingia sehemu ya saba ambayo itakua ni kuweka marumaru eneo la mlango wa Swahibu Zamaan na Imamu Hussein (a.s) upande wa magharibi wa haram tukufu.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi ya Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi hii haijaishia kwenye kuweka marumaru peke yake, kulikua na kazi za utangulizi, kwa ajili ya kuwawezesha mafundi kufanya kazi yao, kulikua na kazi ya kutoa marumaru za zamani, kukarabati kuta na sehemu ya ardhi pamoja na kuweka tabaka la chuma ambalo marumaru zitakaa juu yake, sambamba na kuweka nyaya za umeme, mawasiliano na vipaza sauti, na njia za maji na mengineyo, na kuziunganisha na mitambo mikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kua: “Hakika marumaru mpya zilizo wekwa ni za (Multi-Onx) zimesha fanyiwa majaribio mbalimbali, ni imara na rangi yake haichuji, pia zinasifa nyingine nyingi zinazo sababisha ziwe bora tofauti na zingine”.

Kumbuka kua haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia kutekelewa miradi mingi, iliyo fanywa kwa wakati na sehemu tofauti, mfululizo wa miradi hiyo unahitimishwa na mradi huu wa kuweka marumaru katika haram tukufu, kwa mara ya mwisho kuwekwa marumaru ilikua miaka ya sabini karne iliyo pita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: