Mradi wa kuweka marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upo katika hatua za mwisho, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Swaaigh.
Akasema: “Mafundi na wahandisi ya kitengo tajwa wanaendelea na kazi ya kumalizia hatua za mwisho katika mradi wa kuweka marumaru ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), inakaribiwa kumalizwa kazi zote za upanuzi na ukarabati ya jengo hilo tukufu”.
Akabainisha kua: “Mafundi na wahandisi wanafanya kazi muda wote, kwa ajili ya kukamilisha mradi huu muhimu kwa kila anayekuja Karbala, tunafanya kila tuwezalo kukamilisha mradi wa kuweka marumaru ndani ya haram, katika sardabu na kwenye korido za haram tukufu”.
Akaongeza kua: “Hakika mradi kamili umehusisha kuweka mabomba ya maji, mfumo wa umeme, mfumo wa maji ya baridi yanayo wekwa kwenye madeli yaliyopo ndani ya haram, eneo la mradi linaukubwa wa mita za mraba (5,000)”.
Kumbuka kua mradi wa kuweka marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) unakamilisha miradi mingi iliyofanywa awali, unatekelezwa kutokana na kuharibika kwa marumaru zilizo kuwepo jambo lililo sababisha kuharibika muonekano wake, marumaru hizo zilikua na zaidi ya miaka (50), ndipo Atabatu Abbasiyya ikaamua kutekeleza mradi huu, kwa lengo la kupendezesha mahala hapa ambapo ni sehemu miongoni mwa sehemu za peponi, kwa namna ambayo itapendeza na kufurahisha nafsi ya zaairu mtukufu.