Kitengo cha usimamizi wa kihandisi chakamilisha hatua ya kwanza ya mradi wa kujenga jengo la watoto.

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea na ujenzi wa shule ya watoto, wamemaliza hatua ya kwanza na kuingia hatua ya pili, wamefanya kazi kubwa kukamilisha kazi walizo pangiwa kwa wakati.

Mhandisi ambaye ni kiongozi wa mradi Ustadh Mursil Raafii Al-Aamiriy ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu mradi huu kua: “Jongo la shule za awali (chekechea) linajengwa katika mtaa wa Baladiyya kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba (400), nalo ni jengo la ghorofa mbili kila moja ina kumbi tano za darasa, madarasa ya tabaka la chini ni kwa aliji ya watoto wa masomo ya awali (chekechea), na ghorofa ya kwanza ni kwa ajili ya madrasa ya Darul-Ilmi Diniyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Akaongeza kua: “Kuna vyumba vya huduma tofauti, jiko pamoja na vyoo, na mifumo ya Intanet, viyoyozi na umeme”.

Akaendelea kusema: “Kazi hii ileanza karibu siku hamsini zilizo pita, tumesha kamilisha kazi kwa asilimia %30, hatua ya kwanza imehusisha kujenga msingi na nguzo za tabaka la chini pamoja na kumwaga zege ya dari la tabaka la chini na kujenga nguzo za tabaka la pili”.

Akaashiria kua: “Kazi za hatua ya pili zinazo endelea zinahusisha ujenzi wa tofali”.

Kumbuka kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya kinamchango mkubwa katika miradi mingi ya ujenzi ndani na nje ya Ataba tukufu, kwani kina mafunzi wa aina tofauti waliobobea katika fani mbalimbali za ujenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: