Maoni katika picha
Paa iliyo jengwa imezingatia alama za kiislamu katika ujenzi wa haram za malalo matakatifu, tena imepambwa zaidi, kwa sababu kazi ya kuchagua aina za nakshi na mapambo ya paa na kubba tukufu imefanywa na wajenzi wa kiislamu wanaofahamu mazaru na Ataba tukufu zote, hivyo waliangalia nakshi na mapambo yaliyopo katika Ataba za zamani kisha wakachagua aina bora na nzuri na wakajenga kisasa zaidi.
Kazi hii imefanywa na mikono ya raia halisi wa Iraq, walikua na haki ya kupata nafasi hiyo na kuonyesha uwezo wao, sambamba na vifaa bora na vizuri kabisa vilivyo tumika katika utekelezaji wa mradi huu, yote hayo ni kwa ajili ya kuhakikisha tunatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s).