Watumishi wa kiwanda cha Saqaa wamefika asilimia hamsini (%50) ya kufunga vipande vya juu walivyo tengeneza vya dirisha la Maimamu wawili Aljawadaini (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wanaofanya kazi katika kiwanda cha Saqaa cha kutengeneza madirisha na milango ya kwenye makaburi na mazaru matakatifu, hivi sasa wanatengeneza na kuweka dhahabu sehemu ya juu ya dirisha la Maimamu wawili Aljawadaini (a.s) wamefikia asilimia hamsini (%50) ya kufunga vipande vya dirisha tukufu walivyo tengeneza na kuvitia dhahabu, muda wa mutekeleza mradi huu ni siku (60), hadi sasa wamesha tumia karibu kila (12) za dhahabu na Ayaar 24, pamoja na dhahabu iliyokuwepo tangu zamani katika dirisha tukufu, wanafanya kazi mchana na usiku kwa ajili ya kumaliza ndani ya muda uliopangwa.

Katibu mkuu wa Atabatu Kaadhimiyya tukufu Shekh Ali Kadhimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kaburi la Maimamu wawili Alkadhimaini (s.a), baadhi ya sehemu zake zilikua zimeanza kuharibika, hasa sehemu ya taji linalo zunguka kaburi la Maimamu hao ambazo zimetengenezwa na kuwekwa dhahabu upya”.

Akaongeza kua: “Tulikua tumesha pata uzowefu kwa kutengeneza madirisha mawili la Shekh Mufidi na Shekh Tusi, baada ya kumaliza miradi hiyo tuligundua kitu kipya, ndipo uongozi mkuu wa Atabatu Alkadhimiyya ukaamua kusimamia kazi ya kuweka dhahabu na madini ya mina kupitia kiwanda cha Saqaa kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumepata mafanikio makubwa zaidi ya tulivyo tarajia kutokana na juhudi pamoja na uzowefu walio nao mafundi, kwani wamefanya kazi kwa umakini mkubwa na kwa ubora wa hali ya juu ukizingatia kua kazi hii inawahusu Maimamu wawili Alkadhimaini (a.s)”.

Fahamu kua mkataba wa kuweka dhahabu sehemu ya juu ya dirisha la maimamu wawili Aljawadaini (a.s) ulitiwa sahihi na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar mwezi ishirini na tisa Shabani mwaka (1440h) sawa na tarehe tano mei (2019m).

Kumbuka kua mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaofanya kazi katika sekta ya utengenezaji wa madirisha ya makaburi na mazaru matakatifu wana uzowefu mkubwa na kazi yao, wameweza kuonyesha kwa vitendo ubora wao kuanzia walipo tengeneza dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s), nalo ndio dirisha la kwanza kutengenezwa na raia wa Iraq, kisha wakatengeneza dirisha la Qassim (a.s) na milango ya malalo ya Sayyid Muhammad –Sabú Dujail- na madirisha ya Swafi Swafa, sambamba na madirisha ya Shekh Mufidi na Shekh Tusi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: