Wasifu wa dirisha hilo ni:
- 1- Linaupana wa (mita 6 na sm 6), na urefu wa (mita 3 na sm 25) takriban.
- 2- Kiwango cha madini ya fedha kilicho tumika kinakaribia (kilo 88), na dhahabu ni zaidi ya kilo moja, inakaribia gram (1150).
- 3- Yametumika madini mengine tofauti, ikiwemo (chuma) kopa na mbao bora kabisa.
- 4- Aya iliyo andikwa inatoka katika surat Yunis.
- 5- Limewekwa nakshi za mimea.
Fahamu kua mafundi wa kiwanda cha Saqaa kinacho husika na kutengeneza madirisha na milango ya makaburi na mazaru tukufu wataanza kutengeneza dirisha hilo mwishoni mwa mwezi huu wa Dhulhijja.