Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka kiwanda cha Saqaa kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumatano (12 Dhulhijja 1440h) sawa na (14 Agost 2019m) wameanza kazi ya kuweka dirisha jipya kwenye mazaru ya Qassim bun Imamu Alkadhim (a.s).
Kazi hiyo imeanza baada ya mafundi wa kiwanda hicho kukamilisha kazi ya kuondoa dirisha la zamani na kulikabidhi kwa uongozi wa mazaru hiyo, kwa ajili ya kulihifadhi, na siku za baadae linaweza kuwekwa katika makumbusho ya mazaru hiyo au makumbusho nyingine yeyote miongoni mwa makumbusho za Ataba tukufu.
Mkuu wa kiwanda cha Saqaa Sayyid Nadhim Jaasim Algharabi ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu kuanza kwa kazi ya kuweka dirisha jipya kua: “Baada ya kuwasili dirisha jipya katika mazaru tukufu, leo asubuhi mafundi wameanza kazi ya kuweka dirisha hilo katika mazaru baada ya kumaliza kuondoa dirisha la zamani”.
Akasema: “Dirisha hili kwa nje lina urefu wa (mt 4.70) na upana wa (mt 3.60) na kimo chake ni (mt 4.10)”.
Akaongeza kua: “Kazi itafanywa mfululizo bila kupumzika hadi mafundi watakapo maliza, leo wamemaliza kuweka majengo ya mbao na sasa wataendelea kuweka vipande vilivyo tengenezwa kwa madini mbalimbali”.