Kitengo cha usimamizi wa kihandisi: kinaendelea kijenga kumbi za maabara katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na ujenzi wa kumbi za maabara katika chuo kikuu cha Al-Ameed, hadi sasa wamesha kamilisha asilimia tisini (90%).

Mradi umewekwa vifaa bora vya umeme na mitambo ya kisasa pamoja na vifaa vya maabara, ukubwa wa kiwanja ni mita za mraba elfu moja mia sita.

Msimamizi mkuu wa mradi huo Mhandisi Ali Muhammad Hussein amesema kua: “Jengo lina ghorofa nne, litakuwa na vyumba vya maabara (16) na vyumba vya madarasa (8), hadi sasa mradi umesha piga hatua kubwa, kiwango cha ukamilifu kinakadiriwa kuwa asilimia tisini (90%).

Fahamu kua kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni moja ya vitengo muhimu, kupitia kitengo hicho miradi muhimu ya Atabatu Abbasiyya imetekelezwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: