Hatua ya kwanza ya kufunga dirisha la Maqam ya Imamu Mahdi (a.f)

Maoni katika picha
Maqam ya Imamu Mahdi (a.f) haijashuhudia matengenezo makubwa kama yanayo fanyika hivi sasa, yanayo fanywa na Atabatu Abbasiyya kwa muda urefu na bado yanaendelea, chini ya mkakati wa kuifanya iwe katika muonekano bora na mzuri.

Kutokana na ujenzi huo, mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha na milango ya kweenye makaburi matukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, wameanza hatua ya kwanza ya kufunga dirisha la Maqam takatifu litakalo chukua nafasi ya dirisha la zamani, lililotengenezwa miaka mingi iliyopita jambo ambalo limepelekea kupoteza uzuri wake, na kutoendana na maendeleo ya jengo, dirisha jipya linakamilisha ubunifu wa mafundi wa Ataba tukufu katika eneo hilo, linalo tembelewa na maelfu ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq.

Kiongozi wa kitengo hicho Sayyid Naadhim Gharabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Dirisha la Maqam ya Imamu Mahadi (a.f) linatokana na ubunifu wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), linaingia katika orodha ya madirisha waliyo tengeneza ya makaburi na mazaru tukufu, kwa kutumia kiwanda cha ndani na mafundi wazalendo bila kutegemea msaada wowote kutoka nje”.

Akaongeza kua: “Tumekamilisha kutengeneza vifaa vya umbo la dirisha kwa ubora wa juu, matengenezo hayo yanafanana na yale yaliyofanywa katika dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa nakshi na mapambo”.

Tumeongea na makamo kiongozi wa kitengo hicho Ustadh Husaam Muhammad Jawaad kuhusu wasifu wa dirisha hilo amesema kua: Umbo la dirisha hilo linafanana na dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuna mfanano katika upande wa mapambo na nakshi, mafundi wamelijenga kwa umaridadi na uhodari mkubwa na kuhakikisha linaendana na utukufu wa mahala linapo wekwa, miongoni mwa wasifu wa dirisha hilo ni:

  • - Dirisha lina urefu wa (mt 6) na upana wa (mt.3.5).
  • - Tumetumia karibu (kg 1.15) za dhahabu halisi.
  • - Tumetumia zaidi ya (kg 88) za fedha.
  • - Tumetumia mina za kioo karibu (kg 25).
  • - Tumetumia (kg 700) takriban za silva.
  • - Tumetumia zaidi ya (kg 1500) za chuma.
  • - Tumetumia mbao za Burmiy zinazo endana na uzito wa dirisha.

Akaongeza kua: Muundo wake unamadirisha matano pamoja na mlango wenye maandishi ya beti za mashairi, juu ya maandishi hayo kuna mstari wa (pambo la dhahabu) katikati yake kuna aya isemayo (Na tunataka kuwaneemesha wale waliodhoofishwa katika ardhi na tuwafanye maimamu na tuwafanye warithi) halafu kuna mstari mwingine umeandikwa kutoka katika surat Yunusi aya ya 100 (Na haikua nafsi ni yenye kufa…) hadi mwisho wa aya ya 103 (Hivyo ni haki juu yetu kuwaokoa waumini) na juu yake kuna maua (20) yaliyo pambwa kwa rangi ya dhahabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: