Watu wa Hilla wanaomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Maoni katika picha
Nyoyo zilizojaa huzuni na majonzi, mawakibu za watu wa Hilla zinaomboleza kifo cha mtukufu Ummul-Banina (a.s) mbele ya kaburi la mtoto wake mwezi wa bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s).

Huku sauti za waombolezaji walioshiriki kwenye maukibu hiyo kubwa ambayo hufanywa kila mwaka na watu wa mji huo kwa ajili ya kumpa pole mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s) zikisikika zikisoma kaswida za huzuni kutokana na msiba huo.

Mawakibu hizo zimehitimisha uombolezaji wao kwa kufanya majlisi ndani ya haram ya Abbasi, ambayo kundi kubwa la mazuwaru pia wameshiriki.

Tambua kua bibi mtakatifu mchamungu Ummul-Banina (a.s) alifariki mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar siku ya Ijumaa mwaka wa (64h), miaka mitatu baada ya shahada ya Imamu Hussein (a.s), umri wake aliutumia katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kuvumilia misiba mikubwa ya kufiwa na mawalii wa Mwenyezi Mungu, ikiwa ni pamoja na kufiwa na watoto wake wanne siku ya Ashura pamoja na ndugu yao Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: