Watumishi wa malalo ya mtoto wake wanaomboleza kifo chake

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo (13 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (8 Februari 2020m) imefanywa majlisi ya kuomboleza kifo cha mnusuruji wa kizazi kitakatifu na chemchem ya kujitolea bibi mtukufu Ummul-Banina (a.s), mzazi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ambae tupo katika siku za kuomboleza kifo chake.

Majlisi hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nayo ni sehemu ya utaratibu wake wa kuomboleza msiba huo.

Majlisi hiyo imehudhuriwa na kundi kubwa la watumishi wa malalo ya mtoto wake pamoja na jopo la mazuwaru, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu, halafu ukafuata muhadhara uliotolewa na Mheshimiwa Shekh Muhammad Kuraitwi kutoka kitengo cha Dini, amezungumza mambo mengi kuhusu maisha ya mama huyu mtukufu, na miongoni mwa heshima kubwa aliyopewa na Mwenyezi Mungu amekua ni miongoni mwa milango yake ya Rehema katika kukidhi haja za watu na kuwafanyia wepesi mambo yao.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum kwa ajili ya kuomboleza msiba huu, ratiba ambayo inavipengele vingi vya uombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: