Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s), ndani ya moja ya kumbi za chuo, majlisi hiyo imehedhuriwa na idadi kubwa ya wakufunzi wa chuo na viongozi wake pamoja na wanafunzi, mawaidha yametolewa na Shekh Jafari Dujaili, amezungumzia baadhi ya sifa nzuri alizokua nazo bibi mtakatifu Ummul-Banina (a.s), na akaelekeza namna ya kunufaika na mafundisho yake katika maisha yetu ya kila siku.

Naye rais wa chuo Dokta Nuuris Dahani amesema: “Chuo kikuu cha Alkafeel kimezowea kufanya majlisi za kuomboleza, kwa ajili ya kupata mazingatio na masomo kwa watu wote, ikiwa ni pamoja na kuomboleza kifo cha mama huyu mtakatifu Ummul-Banina (a.s)”.

Dokta Husaam Ubaidi rais wa kitengo cha sheria na maelekezo ya kinafsi na kimalezi amesema kua: “Ngazi ya chuo ni muhimu sana katika kumjenga mtu, kufanya majlisi hizi kunachangia kuwajenga wanachuo, na kuwalinda na kasoro mbalimbali za kifikra”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: