Ratiba mpya: Msafara wa Saaqi unakwenda kutembelea malalo tukufu katika jamhuri ya kiislam ya Iran.

Maoni katika picha
Kitengo cha utalii wa kidini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia msafara wa Saaqi kimetangaza ratiba ya safari ya Iran (kwa njia ya barabara), kumzuru Imamu Ridhwa na bibi Fatuma Maasuma (a.s).

Kwa mujibu wa ratiba iliyo tangazwa safari itakua ya siku kumi na mbili (12), siku tano (5) katika mji wa Mash-hadi na siku tatu Qum, ratiba inahusisha (Viza, usafiri wa magari ya kisasa yenye viyoyozi kutoka Iraq hadi Iran, makazi katika hoteli za kisasa, matembezi ya kila siku, milo mitatu).

Ratiba ipo kama ifuatavyo:

Siku ya kwanza/ kukutana katika barabara ya Maitham Tammaar – kituo cha Saaqi, na kuondoka kwa magari ya kisasa hadi mji mtukufu wa Qum.

Siku ya pili/ Baada ya kuwasili katika mji wa Qum tutakaa katika hoteli za kisasa siku mbili ambazo tutakua tunaenda kumzuru Maasuma (a.s) na kurudi hotelini.

Siku ya tatu/ tutaenda katika Masjid Jamkarani, Baitu Nuur, Mussa Mubarqai na Arbaini Alawiyya (a.s).

Siku ya nne/ tutaenda katika mji wa Mash-had na kuzuru Maqam ya unyayo wa Imamu Ridhwa (a.s) katika eneo la Nishabuur, kisha tutawasili katika mji mtukufu wa Mash-had, na kukaa kwenye hoteli ya kisasa kwa muda wa siku saba.

Siku ya tano/ kutembelea malalo ya Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s).

Siku ya sita/ kutembelea malalo ya ndugu zake Imamu Ridhwa (a.s) Yaasir na Naasir (a.s), halafu tutatembelea eneo la kitalii katika mji wa Twarqabah.

Siku ya saba/ kutembelea malalo ya Sayyid Yahya mtoto wa Zaidi Shahidi (a.s) katika mji wa Mayami.

Siku nane/ mapumziko.

Siku ya tisa/ mapumziko.

Siku ya kumi/ tutaenda katika mji wa Tehran kutembelea malalo ya Sayyid Abdul-Adhim Hassan na Sayyid Twaahir bun Imamu Zainul-Abidina (a.s) na Sayyid Hamza mtoto wa Imamu Mussa Alkaadhim (a.s), kisha kwenda katika mji mtukufu wa Qum na kukaa kwenye hoteli ya kifahari siku moja.

Siku ya kumi na moja/ kujiandaa kurudi katika taifa letu kipenzi, safari itaanza baada ya Adhuhuri kuelekea katika mji mtukufu wa Karbala.

Bei zipo kama zifuatazo:

Mtu mwenye umri wa (miaka 12 na kuendelea) dinari laki mbili (200,000) keshi na lakimbili na elfu ishirini na tano (225000) mkopo.

Mtoto mwenye umri wa (miaka 2 hadi 11) dinari laki moja na elfu sabini na tano keshi, na dinari laki mbili (200,000) mokopo.

Mtoto mwenye umri chini ya miaka miwili bure.

Anaehitaji chumba cha pekeyake ataongeza dinari elfu hamsini (50,000).

Kwa maelezo zaidi au kuoda nafasi tembelea matawi yafuatayo:

Tawi la kwanza/ Babu Bagdad, au piga simu namba (07801952463/ 07602283026).

Tawi la pili/ Mkabala na Babu Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) au piga simu namba (07602327074).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: