Hivi ndio watumishi wa Atabatu Abbasiyya walivyo mpa pole Abulfadhil Abbasi kwa kufiwa na mama yake.

Maoni katika picha
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya Adhuhuri ya siku ya Jumamosi (13 Jamadal-Aakhar 1441h) sawa na (8 Februari 2020m) wamempa pole wanae mtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s), katika kumbukumbu ya kifo cha mama yake bibi mtakatifu Ummul-Banina (a.s), wamesimama kwa mistari mbele ya kaburi lake na kusoma ziara tukufu, ikafuatiwa na wimbo wa (Lahnul-Ibaa) pamoja na tenzi za kuhuzunisha zinazo elezea msiba huo.

Baada ya hapo; kinyume na mazowea, watumishi hoa waliwapokea ndugu zao watumishi wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), waliokuja kumpa pole mfiwa mkuu mwezi wa bani Hashim (a.s) kwa kufiwa na mama yake Ummul-Banina (a.s), hapo wakaungana watumishi wa Ataba mbili ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kufanya majlisi ya kuomboleza iliyo pambwa na kaswida pamoja na tenzi za huzuni, zilizo onyesha maumivu makubwa yaliyopo katika nyoyo za waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Hali kadhalika kundi kubwa la watu waliokuwepo ndani ya haram ya Abbasi na mazuwaru wa Ataba mbili tukufu wameshiriki kwenye maombolezo hayo, chini ya mazingira tulivu yaliyojaa huzuni ya kumpa pole aliyekatwa mikono miwili kwa kufiwa na mama yake Ummu-Banina (a.s).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya siku mbili zilizo pita imepokea makumi ya mawakibu za kuomboleza kutoka ndani na nje ya Karbala, sambamba na maelfu ya watu waliokuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) na kumpa pole kwa kufiwa na mama yake mtakatifu bibi Fatuma bint Hizaam Ummul-Banina (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: