Miongoni mwa mkakati wa Atabatu Abbasiyya ni kuzipa majina baadhi ya barabara zinazo elekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na kuomboleza kifo cha mama yake, moja ya barabara inayo elekea Atabatu Abbasiyya imepewa jina la Ummul-Banina (a.s), inayo anzia kituo cha ukaguzi za Alkafeel kupitia mlango wa Bagdad hadi katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Sayyid Naafii Mussawi kiongozi wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya ambao ndio wapendekezaji wa jambo hili, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kuzipa majina mapya barabara ni miongoni mwa mambo ambayo tumeanza kuyafanya hivi karibuni, tumeanza na barabara hii ambayo kuna waliokua wanaiita barabara ya mlango wa Bagdad na wengine walikua wanaiita barabara ya Ammaarah Ta-amiin au barabara ya Ta-amiin, kutokana na kuwepo kwa jengo katika barabara hii, hali itakua hivyo pia katika barabara zitakazo badilishwa majina siku za mbele”.
Ustadh Swabaahu Faadhil Hanashi amesema kua: “Fikra hii haijaanza leo, japo imeanza kufanyiwa kazi hivi sasa baada ya kuona kuna utata wa majina katika baadhi ya barabara, kuna barabara zenye zaidi ya jina moja, jambo ambalo linamchanganya zaairu”.
Akaongeza kua: “Barabara tuliyoipa jina leo inaurefu wa zaidi ya kilometa moja, sambamba na kubadilisha jina la barabara kuna baadhi ya vituo vya ukaguzi pia vimebadilishwa majina, kama vile kituo cha (Ta-amiin) sasa kinaitwa (Alqamar), jambo hili linafanywa kwa makubaliano na wenye mamlaka ya kisheria”.