Mazuwaru wa kike wanaomboleza kifo cha mama yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya kaburi lake tukufu

Maoni katika picha
(Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo), kutokana na aya hiyo tukufu, idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya imefanya kumbukizi ya kifo cha Ummul-Banina (a.s), ndani ya sardabu ya Imamu Kaadhim (a.s) katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhudhuriwa na kundi kubwa la mazuwaru.

Makamo kiongozi wa idara ya wahadhiri wa kike bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: Idara ya wahadhiri wa kike inazingatia kwa makini utaratibu wa ufikishaji wa ujumbe wa Ahlulbait (a.s) kwa makundi yote ya jamii.

Kuhusu ratiba ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s), amesema kua: “Ratiba yote inalenga kuweka njia ya kufundisha utamaduni wa Husseiniyya katika jamii kwa namna inayo endana na umuhimu wa tabligh katika zama zetu, sambamba na kueleza ukubwa wa jukumu la wahadhiri katika kupambana na vita ya kifikra na kiitikadi inayo shambulia uislamu, akasisitiza pia ulazima wa kushikamana na historia sahihi, na kuchukua elimu katika vyanzo sahihi, sambamba na kua na utaratibu mzuri wa kufikisha ujumbe na wenye kuathiri”.

Kumbuka kua lengo la idara hiyo ni kuboresha tablighi katika upande wa wanawake kutokana na umuhimu wao hasa wakati wa msimu wa maombolezo, kuwatoa pembezoni na kueleza dhulma walizo fanyiwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) kwa kutumia njia salama inayo eleweka na kuendana na uhalisia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: