Kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) kinafanya kumbukumbu ya kifo cha bibi wa kujitolea na uaminifu Ummul-Banina (a.s), kupitia majlisi ya kuomboleza iliyo hudhuriwa na makumi ya wanawake wafuasi wa Ahlulbait (a.s), nalo ni jambo la kiimani ambalo wanawake wa Karbala wamezowea kulifanya katika siku kama hizi za kuomboleza msiba huu mkubwa kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Katika mazingira yaliyojaa huzuni na majonzi wakinamama wamemiminika kwenye kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s), kushiriki katika majlisi ambayo imeelezewa historia ya bibi huyo mtakatifu na msimamo wake uliofanya aendelee kukumbukwa milele kama alama ya huzuni na kujitolea.
Bibi Zainabu Ardawi kiongozi wa kituo cha Swidiqah Twahira (a.s) alipokutana na mtandao wa Alkafeel amesema: Atabatu Abbasiyya siku zote huangalia malengo na kusimamia ukweli wa kihistoria, hivyo imefanya kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s) mama mwenye mafunzo mengi ambayo sisi tunahaja nayo kubwa katika sekta ya malezi na jamii hadi kwenye sekta ya Dini, tukiangalia katika kumuomboleza Ummul-Banina (a.s), tunakuta kua tunahitaji sana kuangalia sekta ya familia na umuhimu wake, pamoja na matatizo ya nafsi, kama alivyo kua Ummul-Banina pamoja na Hassan na Hussein na watoto wake (a.s), katika mnasaba huu tunaweza kueleza mafundisho yanayo patikana kutoka kwake, na tunaweza kutuma ujumbe unaokubalika kwa Ummul-Banina.
Majlisi ikahitimishwa kwa kuimba tenzi za huzuni na kusoma Quráni tukufu halafu thawabu zake zikaelekezwa kwa bibi mtakatifu (a.s).