Idara ya Tahfiidh katika Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya inafanya kikao cha kusoma Quráni ndani ya mazaru ya Alawiyyah Sharifah binti Hassan (a.s) kwa ushiriki wa wanafunzi (120), jambo hilo ni sehemu ya harakati za Maahadi ya Quráni kwenye mikoa tofauti hapa nchini.
Kikao kimefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyosomwa na Haafidh Muhammad Abdul-Amiir Zaamiliy, kikafuata kisomo cha pamoja, kisha wahudhuriaji wakapewa nafasi ya kuwauliza maswali wasomaji wa Quráni ili kuonyesha vipaji vyao.
Kulikua na kipengele cha Quráni tafsiri, ambacho alishiriki Haafidh Ibrahim Ali, na Muhammad Hassan, halafu ikafuata Quráni iliyosomwa na Haafidh Walaa Liith, wakahitimisha kwa kisomo cha pamoja kutoka kwa wanafunzi wa tahfiidh.
Kiongozi wa idara ya Tahfiidh Ustadh Hamza Fatalawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hafla hiyo imehusisha maonyesho ya kuhifadhi Quráni pamoja na namba za kurasa na aya, sambamba na kisomo cha kukimbizana katika hifdh na usomaji wa pamoja”.
Akasema: “Lengo la kufanya vikao hivi ni kuhamasisha kuhifadhi wanafunzi wetu wanaotaka kuzama katika kitabu kitakatifu”.
Kwa upande wao wanafunzi wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia Maahadi ya Quráni tukufu, kwa kuwapa fursa ya kushiriki kwenye hafla hii, wakasema kua huo ni mwanzo wa kuelekea kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa.