Watumishi wa idara ya kuwasaidia wenye mahitaji maalum na wenye umri mkubwa chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, wanafanya kazi nzuri sawa na watumishi wengine, wote kwa pamoja wanatoa picha nzuri kwa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Wakati wa joto la kiangazi na baridi la masika utawakuta watumishi hao wamesimama wakisubiri kutoa huduma huku wakiwa na tabasamu, kila mmoja anaomba ampate mzee au mgonjwa ili ampokee na kumpeleka kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), bila kujali mazingira magumu ya hali ya hewa, kwa kutumia viti maalu vya mataili vilivyo andaliwa rasmi kwa kazi hiyo na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Idara hiyo inazamu mbili (asubuhi na jioni) kila zamu wanafanya kazi saa saba, jukumu lao ni kubeba watu wenye mahitaji maalum na wazee wenye uhitaji wa kusaidiwa katika kufanya ziara.
Watumishi wa idara hiyo wamekaa katika milango ya kuingia ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanajukumu la kuwabeba mazuwaru wanaohitaji kutumia viti vya mataili kuanzia sehemu zinako ishia gari za abiria hadi kwenye haram tukufu, pamoja na kuwaingiza ndani ya haram na kuwasaidia kufanya ibada ya ziara, imeandaliwa njia maalum na sehemu rasmi kwenye dirisha takatifu kwa ajili yao.