Kuanza kwa hatua ya kwanza ya mradi wa (mlango wa Haja za wakazi)

Maoni katika picha
Idara ya Samawa chini ya ofisi ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya, imeanza hatua ya kwanza ya mradi wa (mlango wa haja za wakazi) unaolenga kusaidia familia za mafakiri katika mkoa wa Muthanna, kupitia program ya kibinaadamu inayo tekelezwa na idara hiyo.

Kiongozi wa idara Sayyid Jaabir fadhwalah ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mradi uliotangazwa hapo kabla unalenga kuwapatia makazi mazuri familia zisizokua na nyumba au zisizokua na makazi mazuri, jambo hili linatekelezwa chini ya program ya kibinaadam inayofanywa na idara tajwa”.

Akaongeza kua: Eneo la ardhi iliyotengwa kwa ajili hiyo linaukubwa wa (mita za mraba elfu tano 5000) patajengwa nyumba (24) pamoja na msikiti na bustani.

Akabainisha: kabla ya kuanza hatua ya kwanza ya kusawazisha kiwanja, tumechukua vibali vyote vinavyo hitajika kutoka serikali ya mkoa.

Akasisitiza kua: “Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na juhudi za wahisani, siku za mbele tutashuhudia kuanza kutekelezwa hatua inayo fuata, na kukamilishwa kwa wakati, jambo litakalo saidia kuingiza furaha kwa familia nufaika”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: