Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya yafanya shindano la khutuba ya bibi Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya inatangaza shindano la kusoma khutuba ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s), aliyotoa kwa wanawake wa Muhajirina na Answari.

Shindano hili ni sehemu ya kuadhimisha turathi za Ahlulbait (a.s) pamoja na kubainisha dhulma aliyo fanyiwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Kila mwanamke anaruhusiwa kushiriki katika shindano hili, na atatakiwa kujibu kwa:

  • 1- Kuhifadhi maana ishirini za maneno ya Khutuba.
  • 2- Kuandika nakala ya khutuba.

Kuchagua jibu sahihi katika maswali matano mwishoni mwa shindano.

Wakati wa jaribio: Jumanne ya kwanza katika mwezi wa Rajabu saa tatu na nusu asubuhi.

Sehemu ya jaribio: Ghorofa la chini liitwalo Imamu Ali Haadi katika Atabatu Abbasiyya karibu na mlango wa Furaat (namba 8).

Zawadi za washindi: Mshindi wa kwanza atapata dinari laki moja na nusu (150,000) baada ya matokeo ya kura, washiriki wote waliojibu vizuri watapewa pete kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maswali maalum katika shindano la Fatwimiyyah:

Swali la kwanza: Bibi Fatuma Zaharaa (a.s) alikusudia nini alipotoa ushahidi wa aya hii (Hiyo ni hasara ya wazi)?

1/ Hasara ya vitu au dini?

2/ Hasara ya dunia au akhera?

3/ Yote mawili ni sawa.

Swali la pili: Imekuaje akachezea ujumbe..!

  • 1- Alishangaa wao kuchagua vibaya! Vipi ukhalifa wa Mtume (s.a.w.w) uondoshwe mahala pake.
  • 2- Zaharaa (a.s) alitaka kubainisha kua ukhalifa ni haki iliyothibiti ndani ya Quráni.
  • 3- Alitaka kubainisha hali ya umma baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).

Swali la tatu: Wamekamua damu katika vyombo vya maziwa.

  • 1- Ishara yake (a.s) kua walikua wanakunywa damu.
  • 2- Kwamba wanajaza damu katika matumbo yao badala ya chakula.
  • 3- Alikutana na fitna gani, wanakamua damu badala ya maziwa.

Swali la nne: Pamoja na watu kutoridhika nao wanadhani wanafanya vizuri?

  • 1- Lengo la maneno yake (a.s) kuwakumbusha wanawake baadhi ya mambo.
  • 2- Alikua hakusudii jamii ya zama zake, bali jamii zingine.
  • 3- Alikua anaonyesha udhalili na kushindwa kwa umma, huku wakidhani kua wameongoka.

Swali la tano: Swidiiqah Twahirah bibi Fatuma Zaharaa (a.s) alisoma aya ngapi katika khutuba yake tukufu?

  • 1- Aya sita katika sura zifuatazo: Maaidah, Aáraaf, Zumar, Hadiid, Yunus, Huud, Zumar.
  • 2- Aya nne katika sura zifuatazo: Aáraaf, Hadiid, Zumar, Maaidah.
  • 3- Aya tatu katika sura zifuatazo: Zumar, Maaidah, Huud.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: