Kuanza kwa hatua za awali katika kufunga dirisha la Swafi Swafa

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wameanza kazi ya kufunga pete ya kaburi la mja mwema Athiba Alyamani ajulikanae kama (Swafi Swafa) –r.a- katika mji wa Najafu ambayo inafungwa juu ya kaburi tukufu, baada ya kumaliza kufunga umbo la mbao na sehemu za madini pamoja na mapambo na nakshi za maandishi ndani ya paa la dirisha hilo.

Kazi ya uwekaji wa marumaru imekamilika kwa kuweka marumaru ya asili (Malt Oxsi) ambayo anaubora mwingi, kwanza ni ya alisi yenye rangi ya kawaida na uwezo wa hali ya juu wa kuvumilia mabadiliko ya hali ya hewa, inaunene wa (sm 4) takriban, imefunika eneo la ndani lenye ukubwa wa (sm 467) kwa urefu na upana wa (sm 355).

Kazi za awali zimefanyika sambamba na uwekaji wa marumaru za (Malt Oxsi) zinazo zunguka umbo la mbao kwa chini, jumla ya vipande hivyo ni (14) vina urefu wa kati ya (sm 100) na (sm 111) na kimo cha (sm 25), kila kipande kinaendana na sehemu kinapo wekwa katika dirisha, umezingatiwa mfanano wa rangi kati yake na marumaru zilizo wekwa maeneo yanayo zunguka hapo, pamoja na eneo la ndani ya dirisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: