Watumishi wa kaburi la ukarimu na kujitolea la, malalo ya mwezi wa familia (a.s), wanaendelea na kazi zao mbalimbali za kuwahudumia mazuwaru watukufu wanaokuja Karbala, miongoni mwa majukumu yao ya kawaida ni kuosha na kuweka manukato katika haram takatifu kwa ajili ya kuweka harufu nzuri kwa mazuwaru.
Kuhusu kazi waliyofanya hivi karibuni ndani ya haram tukufu tumeongea na kiongozi wa idara hiyo, Ustadh Zainul-Aabidina Adnani Ahmadi, amesema kua: Idara yetu imepata utukufu kwa kuosha haram takatifu na kuweka manukato, kazi hiyo tulianza kuifanya saa sita usiku, kwa sababu ya kupungua msongamano wa mazuwaru katika muda huo, tukamaliza saa kumi asubuhi”.
Akaongeza: Watumishi wa idara yeru walianza kusafisha mapambo yaliyopo karibu na kaburi takatifu, pamoja na kuosha vioo na maraya, kisha wakaosha dirisha takatifu na sehemu zote zinazo zunguka haram.
Akamaliza kwa kusema: Baada ya kumaliza kuosha tulianza kazi ya kutia manukato, katika dirisha tukufu na haram kwa ujumla pamoja na kutandika mazulia mapya.