Safari ya kushughulikia kaburi takatifu imechukua siku kumi (10).

Maoni katika picha
Tarehe (7 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (2 Februari 2020m) mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha na milango ya makaburi matukufu chini ya Atabatu Abbasiyya wametangaza kukamilika matengenezo ya dirisha la malalo ya Athibu Alyamani ajulikanae kama (Swafi Swafa) –r.a- katika mkoa wa Najafu, nao ndio waliosimamia usanifu na utengenezaji wake.

(8 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (3 Februari 2020m) vipande vya dirisha viliwasili kutoka Karbala.

(9 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (4 Februari 2020m) mafundi walianza kazi ya kufunga dirisha kwa kutengeneza jengo la mbao ambalo ndio sawa na msingi unaobeba vipande vyote vya dirisha.

10 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (5 Februari 2020m) mafundi walimaliza hatua muhimu ya kutengeneza jengo la mbao, ambayo ni kufunga nguzo kuu na kuzisimika ardhini kwa kufuata tahadhari zote za kihandisi katika kazi hiyo muhimu.

(11 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (6 Februari 2020m) dirisha la Swafi Swafa likashuhudia kufungwa kwa vipande vya kwanza vyenye madini.

(12 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (7 Februari 2020m) rais wa kitengo cha kutengeneza madirisha na milango ya kwenye makaburi –ambao ndio watekelezaji wa mradi huu- Sayyid Nadhim Gharabi akatangaza kua kazi ya kufunga dirisha la Swafi Swafa inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika kwa wakati.

(13 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (8 Februari 2020m) mafundi walikamilisha kufunga ufito wa mapambo yenye dhahabu uliopo sehemu ya juu ya dirisha.

(14 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (9 Februari 2020m) walimaliza kufunga vipande vyote vya madini katika dirisha la Swafi Swafa.

(15 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (10 Februari 2020m) mafundi walimaliza kuweka maandishi yote ya Quráni na mashairi pamoja na mapambo na nakshi za ndani ya dirisha hilo.

(16 Jamadal Aakhar 1441h) sawa na (11 Februari 2020m) kazi ya kuweka sanduku la dirisha la Swafi Swafa ikaanza.

Kazi bado inaendelea hadi watakapo maliza kufunga kila kitu katika dirisha la mja mwema Athibu Alyamani ajulikanae kama (Swafi Swafa) –r.a- katika mkoa wa Najafu, ndani ya muda uliopangwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: