Tawi la Maahadi ya Quráni tukufu katika mji wa Najafu linaendelea na vikao vya usomaji wa Quráni

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati zinazolenga kueneza utamaduni wa kushikamana na mafundisho ya Quráni, Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, linaendelea na vikao vya ufundishaji wa kusoma Quráni kwa ufasaha ambapo walimu wengi na wahitimu wa shule za sekula wanashiriki.

Vikao hivi ambavyo tangu vianze vinazaidi ya mwaka mmoja na nusu vinahusisha ufundishaji wa sifa za herusi za kiarabu, na nyeradi pamoja na usomaji sahihi katika swala, sambamba na nyeradi za mwezi mtukufu wa Ramadhani, na hukumu za nuni sakina na tanwini, pamoja na matamshi ya herufi.

Tunafanya hivyo kwa ajili ya kuandaa walimu wenye uwezo mkubwa wa kufundisha hukumu za usomaji wa Quráni tukufu, katika jamii ya waislamu hapa nchini.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kubinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hufanya semina na warsha za Quráni pamoja na vikao vya usomaji wa Quráni, kama sehemu ya harakati zinazo lenga kutengeneza kizazi cha watu wanaofanyia kazi mafundisho ya Quráni katika taifa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: